Posts

Showing posts from September, 2016

Wema Sepetu Amkataa Idriss Sultan Mchana Kweupeee Pee!

Image
Wema amkataa Idriss Mchana kweupeee pee!!!!! Ashasema hataki kuwa nae sasa nyie endeleeni kupost ohh shem shem sijui kamuoa dada yenu au???? Watabaki kuwa marafiki kama zamani tuuuu...wema so wamchezo mchezooo... unalakusema hapo mdau ???Habari ndo hiyooo... Tukutane katika uwanja wa comments. .. Soma Alichoandika Mtandaoni:

Makahaba Arusha Wamiminika Kujifunza Kiingereza Kuvutia Wateja wa Kigeni

Image
Wasichana wanaojiuza jijini Arusha, wanalazimika kutafuta madarasa ya kujifunza kimombo kwakuwa ni lulu katika maisha ya kazi yao hiyo. Ni kwasababu wale wanaojua Kiingereza hupata wateja wa kigeni ambao hutoa dau kubwa zaidi kwa huduma wanayopewa kuliko wateja wa nyumbani. Mwandishi wa BBC Swahili, Humphrey Mgonja alisafiri hadi Arusha na kushuhudia jinsi biashara hiyo inavyokwenda kwenye mji huo wa kitalii. Alizungumza na msichana anayefanya kazi hiyo aitwaye Warda aliyekiri kuwa Kiingereza kina umuhimu mkubwa kwenye biashara yake. “Sometimes nakutana na wateja ambao hawajui Kiswahili kabisa, unakuta anakuwa ananiongelesha, nasikia lakini nashindwa jinsi ya kumjibu. Kwahiyo nakuwa nakosa hela,” anasema Warda. “Sehemu kama Dar es Salaam niliona sehemu moja kwa Macheni, niliona kuna mademu waliokuwa wanajua Kiingereza walikuwa wanatoka na wazungu. Mimi sometimes wazungu walikuwa wananipenda lakini kwa colour yangu the way nilivyo lakini tulikuwa tunashindwa yaani ni lugha gongana. Kwah...

Picha Mpya za Mrembo Lulu Diva...

Image
Upcoming actress, Lulu Diva has shared her amazing pics of herself on Instagram account, Diva lulu who is so beautiful and has nice figure, see her another pics of herself as she shared on her Instagram account;

Lulu Diva Amdhalilisha Tiffah Wa Diamond

Image
Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kumdhalilisha mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’ kwa kumuita mbwa wake jina Shikiki, ambalo pia ni jina jingine la utani la mtoto huyo. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mrembo huyo amemuita mbwa wake huyo jina hilo, kitu ambacho kimetafsiriwa na wengi kama ni kumdhalilisha mtoto huyo wa staa mkubwa Bongo. “Jamani Diva anatafuta matatizo makubwa na D i a m o n d , kwanini kampa mbwa wake jina kama hilo ambalo pia huwa linatumiwa na Tiffah? Ana hatari sana,” kilisema chanzo chetu. Gazeti hili lilipomtafuta Lulu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, alisema ni kweli mbwa wake anaitwa Shikiki lakini hakuwa akijua kwamba mtoto wa Diamond, jina lake lingine ni hilo. “Jamani mimi sikuwa najua kabisa kama Tiffah, jina lake lingine ni hilo, mimi nilimpa tu kama watu w e n g i n e wanavyowapa m a j i n a mbwa wao,” alisema Diva. JE ULIPITWA NA SHAMRASHAMRA ZA MWENGE SINGIDA?? NIMEKUSOGEZEA...

Kupatwa Kwa Mrembo Huddah: Azama Kimapenzi Kwa Mchagga!

Image
Haya jamani yule Sosholaiti wa Kenya kazama kwa Mchaga wa Kishumundu (Sina uhakika). Kaka huyo ajulikanaye kama Danford Kessy amemteka mrembo huyo ambaye amekiri kuwa ni muda mrefu amekuwa akijilinda lakini sasa amefika bei kwa Mkaka huyo Handsome Tazama Picha ya mwanaume huyo hapa:

Chidi Benz Akanusha Kurudia Kutumia Unga...Awatupia Lawama Wabaya wake

Image
  Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amekanusha taarifa ambazo zimezagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amerudia katika matumizi ya Madawa ya kulevya. Rapper huyo amedai taarifa hizo zinasambazwa na wabaya wake ambao hawamtakii mema. “Watu wananipenda kuliko kawaida, hata hayo maneno sijui nimerudia kwenye madawa ya kulevya yaani hata hawajali kabisa ila maadui zangu ndiyo wanajali maneno ila watu wangu hata nikitoka sina nguo wao wanaona mimi nimevaa nguo na watabisha hivyo yaani, hayo maneno wanayosema karudia nawaambia kuwa nirudie nisirudie, nifanye nisifanye sijali, mimi nafanya kazi ambayo wananchi walinijua kupitia kazi hii hivyo siwezi kuharibu hata kidogo, nitumie nisitumie sitakosea kufanya ile kitu wananchi walinijua nikifanya” Chid Benz alikiambia kipindi cha kipindi cha Planet Bongo. Rapper huyo kipindi cha nyuma alikuwa akitumia madawa ya kulevya na baadaye alipelekwa rehabu kwa ajili ya kuacha matumizi ya madawa hayo.

Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12

Image
  Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe. Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume. Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa. Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imes...

Stori ya Kusikitisha ya Mwanamuziki Rah P Baada ya Kuwa Mapenzini na Mwanamume Muuza Madawa ya Kulevya

Image
  Ni stori ambayo aliitoa kipindi cha nyumba kidogo lakini leo nimeona niwaletee na ninyi mtazame akielezea kilichomkuta na mpaka kupotea kabisa katika anga za muziki wa Bongo Flava.....Its so touching yaai i cant watch this twice. she is a good woman, really strong african woman i like her style, naona rap style yake imebadilika. i like the song Ushaurinwa bure, I think she can do wonders akifanya talk show. there are so many women going through such paths, imagine hearing these stories from Tanzanian women waliopo Tz

Hatimaye Baraka Da Prince aikanusha skendo ya Mr Blue kumpigia simu Naj

Image
Msanii Baraka The Prince amezungumzia sakata la mpenzi wake Najma na Mr. Blue ambaye alikuwa mpenzi wake, na kusema tukio hilo halikuwa na ukweli wowote na hata kama lingekuwepo, hawezi kuzuia wawili hao kuwasiliana. Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20 cha East Africa Radio, Baraka amesema yeye hawezi kuzuia wawili hao kuwasiliana kwani wote ni wasanii, na pia hana kawaida ya kushika simu ya mpenzi wake na kujua amewasiliana na nani. “Hamna zile stori sio za kweli, hata mimi Blue alivyoniface nilimwambia sijui hizo habari na sijawahi kuona ukimpigia, hata ukimpigia we ni mwanamuziki mwenzake, mi siwezi nikamuwekea mipaka Najma, au eti siwezi kuwekea mipaka hey Bro usimpigie Najma, kwanza mi hata kugusa tu simu ya Najma sijawahi na hata Najma kugusa simu yangu hagusi yangu, haijawahi kutokea tu kitu kama hicho sasa sijui kilitokea wapi”, alisema Baraka the Prince. Baraka aliendelea kusema ingawa tukio hilo liliathiri kwa upande mwingine, lakini alijaribu kukaa...

Tanzania yaongoza Duniani Kwa Utoaji wa Huduma za Kifedha kwa Kutumia Simu

Image
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu. Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). “Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema. Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo. “Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao um...

Mwanamuziki Vanessa Mdee Ataja Ndoto yake Katika Muziki wa Bongo Flava

Image
Mwanamuziki wa kike anayesumbua ndani na nje ya Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema ana ndoto kubwa. Ndoto yake siku moja, kuwa msanii kutoka Tanzania atakayeshinda tuzo za heshima, Grammy.Anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia. Vee Money ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz. Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo. Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge. “Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo.” amesema Vanessa. Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao.

WCB Waonyesha Jinsi Walivyomalizana na Uongozi wa Saida Karoli ili Kurudia Wimbo wa Salome

Image
Sallam kutoka WCB ameonyesha baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli katika wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’. Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000. Hali hiyo iliufanya uongozi wa Diamond kuzungumza na uongozi wa Saida Karoli ili upate kibali cha kutumia sehemu za nyimbo hiyo. “Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram. “Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,” Diamond kupitia wimbo huu amerudi tena katika nyimbo za asili baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Mdogo Mdogo’ miaka miwili iliyopita.

LULU Michael Atangaza Kuhitaji Kupata Mtoto....

Image
Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael amedai kuwa anahitaji mtoto kwa sasa. Muigizaji huyo ameandika ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram akimuomba Mungu huku akidai kuwa yupo tayari kwa sasa na anahitaji mtoto. “Okay…I’m ready noooow😫😫😫😫and I want a Baby Boy😭😭😫In Jesus Name🙏,” ameandika Lulu kwenye mtandao huo. Kwa sasa muigizaji huyo yupo kwenye mahusiano na bosi wa EFM, Majay. chanzo: UDAKU SPECIAL

Ndege moja kati ya mbili za ATCL Alizonunua Rais Magufuli Itatua Kesho Nchini

Image
Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia  nchini kesho ikitokea Canada. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana. Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada. “Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha.

Tegeta Escrow: TANESCO Yashindwa Kesi Dhidi ya IPTL...Yaamriwa Kulipa Zaidi ya Sh. Bilioni 320

Image
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeshindwa kwenye kesi yake IPTL -Independent Power Tanzania Limited. Hukumu hiyo imefikiwa mwisho wa wiki iliyopita ambapo World Bank tribunal (international centre for settlement of investment disputes. ICSID imeamuru TANESCO kuilipa Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK) kiasi cha dola za kimarekani milioni 148.40 pamoja na tozo riba. SCB HK ndio walionunua mkopo wa IPTL kutoka bank ya Malaysia Danaharta kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 76.1 Kwa habari zaidi soma the Guardian la leo:

Saidi Mamba, mkazi wa Mandewa, Manispaa ya singida anyofolewa sehemu ya ulimi na Mwanamke wakinyonyana ndimi

Image
Kijana Said Mamba, mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, amelazwa hospitali baada ya kung’atwa sehemu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi. Tuandikie maoni yako kuhusu hili.

Serikali yaanza mazungumzo ya kuwaokoa madereva 12 waliotekwa Kongo

Image
Waasi hao mbali na kuwateka madereva hao wametoa saa 24 kuanzia juzi saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Marekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, alisema waasi hao wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha hadi kufikia jana saa 10 jioni. Mindi alisema katika tukio hilo, madereva wawili wa Kitanzania walifanikiwa kutoroka na ndiyo waliosaidia kutoa taarifa kuhusu tukio hilo. “Serikali imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo Jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jana (juzi) Septemba 14, 2016. Kati ya malori hayo manane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa Kitanzania, Azim Dewji na mengine yanamilikiwa na wafanyabiashara kutoka Kenya. “Kwa taarifa zilizopatikana watekaji ni kikundi cha waasi cha Mai Mai ambao baada ya kuyateka magari hayo, waliwashusha madere...

Kanitafutia Kazi Sasa Nimekua Mtumwa wa Ngono Kwake

Image
Hi guys, niaje? Ni miezi miwili sasa tangu nimeacha kazi kampuni ya zamani, na sasa nipo kwenye kampuni nyingine, hii kazi mpya nimetafutiwa na Boss wangu ambae ndie mkuu wa idara yetu, nimepanda cheo kidogo, kule nilikuwa Karani na huku kupya mimi ni Supervisor. Sasa huyu Boss alieniingiza kazini nimekua na urafiki nae tangu nimeingia hapa, kitu kinachonikwaza ni mwenendo wa huyu Boss wangu, yaani nimekua kama mtumwa, wakati wote anataka tufanye ngono, jioni wakati wa kuondoka anataka tubaki ofisini kwake, najikuta nafika home saa tatu hivyo kumkuta Mr wangu amesharudi Muda, inakua ugomvi, inabidi nimdanganye kuwa kazi mpya imekua too demanding kwangu, nachelewa kutoka. Weekend ni hivyo hivyo, inabidi nisingizie home kuwa tunatakiwa kazini hata Jumapili, nimejikuta naishi kama mtumwa kwa sababu ya hii kazi aliyonipa huyu Boss, maneno maneno yamekua mengi hapa kazini miongoni mwa Staff wenzangu kuhusu mwenendo wangu na huyu Boss, nina wasi wasi maneno haya yanaweza kumfikia Mr wangu ik...

Congo DRC: Waasi wa Mai Mai wamewateka madereva 5 wa Tanzania, wanataka $ 4,000 kwa kila Dereva

Image
KUNA TAARIFA KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa deadline ya majeshi kuondoka pia. Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka. TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tan...

Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete

Image
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao. Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki. “Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

EDWARD Lowassa Ampongeza Rais John Pombe Magufuli

Image
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi. Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri. Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta. Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA. Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani. Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dal...

Sanamu Mpya za Mugabe Zazua Ubishi Zimbabwe

Image
Sanamu mbili mpya za kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe Robert Mugabe zimezinduliwa mjini Harare. Sanamu hizo, ambazo zilizinduliwa katika ikulu ya rais zimetayarishwa na mchongaji sanamu maarufu Dominic Benhura. Rais Mugabe ameeleza kufurahishwa na sanamu hizo mbili kwa mujibu wa gazeti la serikali The Herald. "Hii ni kazi nzuri Sanaa ya Sanaa na wasanii walioshiriki inaonekana wana vipaji adimu, wana vipaji kwa kweli," amenukuliwa Bw Mugabe. Bw Benhura ameoneshwa kwenye picha zilizochapishwa na gazeti la The Herald akiwa amesimama karibu na sanamu hiyo akiwa na Bw Mugabe na mke wa rais Dkt Grace Mugabe. Sanamu hiyo, ambayo urefu wake ni karibu maradufu kimo cha Rais Mugabe, inamuonesha kiongozi huyo wa umri wa miaka 92 akiwa na miwani yake maarufu, masharubu na akiwa ameinua mkono akiwa ameufumbata kama ngumi. Baadhi ya raia nchini Zimbabwe hata hivyo hawajapendezwa na sanamu hizo na wanasema zinaonekana kama vibonzo. "Robert Mugabe ametukanwa kwa sanamu hii na bado ha...

Wanafunzi Wacharaza Viboko Walimu Wao, Mmoja Ang'olewa Meno Matano, Mwingine Ngeu Kichwani

Image
Wawanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka “Membele'‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho. Walimu hao wawili wamedai kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe ambapo Mwalimu Gabriel Kambona aliachwa na ngeu kichwani. Mei mwaka huu, Ng’oka “Membele” alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Novemba 2015 na Aprili mwaka huu. Ilisemekana kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano sasa wako Kidato cha Sita katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake. Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu h...

Utendaji Makini wa Mh Rais Magufuli Wapaisha Sekta ya Utalii

Image
Utendaji wa JPM waipaisha sekta ya utalii Uchambuzi wa kina wa hali ya mambo katika sekta moja muhimu ya utalii, eneo linaloiingizia Serikali takribani asilimia 25 ya fedha za kigeni, unaonesha, pamoja na kelele za hivi karibuni, watalii wengi wameongezeka nchini hasa katika kipindi cha Julai mpaka Agosti mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 11. Uchunguzi zaidi umeonesha kuwa watalii wengi waliokuja nchini au wanaofikiria kuja nchini hawajaguswa na ongezeko hilo la kodi zaidi ya kujali aina ya vivutio vilivyoko nchini, hali ya amani na wapo wanaovutiwa pia na utawala wa Rais John Pombe Magufuli ambaye anasikika duniani kote hivyo wanakuja kuona hali ya siasa nchini. Katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, takwimu za watalii waliotembelea hifadhi hiyo, kwa kipindi cha Juni hadi Agosti, 2015 na Juni hadi Agosti, 2016 nako zinaonesha ongezeko. “Kwa kulinganisha idadi ya watalii waliotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kwa miezi mitatu (Juni-Agosti 2015) na mwaka Juni hadi Agosti,2016, inao...

Siwezi Kuyarudia Matapishi Niliyoyatapika - Mr Blue

Image
Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Mboga Saba' amefunguka na kusema kuwa saizi yeye ni mtu mzima anaangalia maisha yake na familia yake hivyo hawezi kurudia matapishi ambayo tayari alishakwisha yatapika. Mr Blue alisema haya kupitia kipindi cha eNewz ya EATV alipokuwa akifafanua juu ya taarifa zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa alimpigia simu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Naj ndipo hapo aliposema hawezi kurudia matapishi aliyokwisha yatapika. "Niliongea na Baraka The Prince alisema kuwa wao hawakufanya hilo jambo, lakini kama wangekuwa ni wao lazima ningetafuta njia ya kuwashikisha adabu maana huko ni kuharibiana. Mimi saizi nimeshakuwa mtu mzima siwezi kurudia matapishi ambayo nilishakwisha yatapika mwanzo' alisema Mr Blue.

Operesheni Dadapoa, Kakapoa Dar es Salaam Yashika Kasi

Image
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linafanya operesheni ya kuwakamata wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanaofanya biashara kinyume cha sheria. Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, ilisema wamebaini baadhi ya nyumba za kulala wageni zinatumika kuhifadhi magenge ya majambazi na wahalifu wengine. Alisema nyumba hizo zimekuwa zikitumiwa na wanawake na wanaume wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘dadapoa’ na ‘kakapoa’. “Ni wajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, hoteli, migahawa, vilabu vya vileo, kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema. Katika hatua hiyo, Kamishna Sirro aliwatahadharisha wafanyabiashara wa nyumba hizo kufuata utaratibu wa kupokea wageni kwa kuandika majina yao kwenye vitabu, namba za vitambulisho vyao na sehemu wanapotoka na pale watakapomtilia shaka mteja yeyote watoe taarifa kituo...

Sijamuimba Siwema wa Nay wa Mitego – Dogo Janja

Image
Msanii Dogo Janja ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kidebe’ na kuwa gumzo mtaani kutokana na kuwasifia baadhi ya wasanii huku wengine akiwaponda, ambapo ndani yake amemtaja mtu anayeitwa ‘Siwema’. Dogo janja ametoa ngoma hiyo wakati wimbo wake wa ‘My Life’ ukiwa badi ni miongoni mwa ngoma ambazo mashabiki wengi wanazikubali huku wengi wao awali wakidhani kuwa asingeweza kufanya wimbo mwingine zaidi ya huo, eNewz ilitaka kufahamu kuhusiana na chanzo cha Dogo janja kumsema Siwema ambaye anajulikana alikuwa ni mpenzi wa rapa Nay Wa Mitego na kubahatika kuzaa naye mototo mmoja kwa kusema “Siyo kiburi siyo mchafu kama Siwema” katika ngoma hiyo. Dogo Janja aliamua kujitetea kuwa Siwema aliyemtaja katika ngoma hiyo siyo Siwema wa Nay wa Mitego bali ni msichana mwingine kutoka Arusha mtaa wa Ngarenaro. Pia alifafanua zaidi kuwa wapo wengi wanaoitwa Dogo Janja lakini sio Dogo janja yeye. “Mimi sijamzungumzia Siwema wa Nay wa Mitego, Siwema pale mtaani kwetu Ngarenaro kuna mwanamke an...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akagua makazi yake mapya Dodoma

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi. Katika ziara hiyo aliyoifanya jana mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika. “Nimekuja kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi watakuwa wamekamilisha,” alisema. Alisema kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu yako Dodoma. Alisema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU. “Tangu wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundomb...

RAIS Magufuli Atonesha Donda la Mbowe

Image
RAIS John Magufuli amepongeza hatua ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kumwondoa Freeman Mbowe, katika jengo ambalo amekuwa akipanga kwa muda mrefu, anaandika Pendo Omary. Siku tano zilizopita, Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia Mbunge wa Jimbo la Hai aliondolewa kwenye jengo hilo na mawakala wa NCH, Fosters Auctioneers kwa madai ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. 1.3 Bilioni huku mvutano wa kuwepo kwa uhalali wa deni hilo ukiendelea. Jengo hilo lipo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam ambapo mawakala hao walichukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji Gazeti Tanzania Daima chini ya Kampuni ya Free Media. Rais Magufuli alilisifu shirika hilo leo asubuhi wakati akizungumza na baadhi ya waliokuwa wapangaji katika nyumba za NHC zilizokuwepo Magomeni Kota ambazo zilibomolewa mwaka 2012. Kwenye mkutano huo Rais Magufuli amelitaka shirika hilo ndani ya siku saba kuwaondoa wapanga...

Mifuko ya hifadhi ya jamii kujenga viwanda vitakavyoajiri asilimia 40 ya Watanzania

Image
Shirikisho hilo limesema litajenga viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vitakavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini ili kupanua wigo wa ajira kwa watanzania. Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Meshack Bandawe amesema baadhi ya viwanda hivyo vitajengwa na mashirika hayo na vingine vitajengwa na shirika moja moja kulingana na maeneo na upatikanaji wa rasilimali na kipaumbele kitatolewa kwa viwanda vya nguo, sukari, vipuri, chai na madawa. Kabla ya shirikisho hilo kutangaza azma hiyo ya kujenga viwanda, shirikisho hilo lilikutana na mawaziri wa wizara za viwanda, biashara na uwekezaji,kilimo,mifugo na uvuvi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge,vijana, ajira na walemavu, afya na maendeleo ya jamii,wanawake wazee na watoto, ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa ambazo baadhi ya mawaziri wake wameridhia mpango huo. Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia ushauri wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa mashiriki ya hifadhi ya jamii kuwa yanapaswa kuanza kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda na sio...

Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi, Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu

Image
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika mkoa wa Dar es Salaam, wameuawa na majambazi wenzao katika eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Licha ya kuuawa kwa majambazi hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamatwa watu zaidi ya saba, wanaosadikiwa kuhusika na tukio la majibizano ya risasi na polisi, lililotokeo Vikindu lililosababisha kifo cha askari mmoja. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro alisema kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya Mbagala, Keko na Kawe jijini humo. Alisema watu hao walikamatwa kufuatia tukio la ujambazi, lililotokea Agosti 29, mwaka huu katika Jengo la Sophia House maeneo ya Veta Changombe, ambapo majambazi hao walidaiwa kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah lenye namba bandia T 549 BPK. Aliongeza kuwa uc...