Posts

Showing posts with the label MAHUSIANO NA NDOA

Serikali yapiga marufuku kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa

Image
Serikali   imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini. Pamoja na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa na   takwimu sahihi   za   vizazi na vifo ama ndoa   inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo. “Wenzetu nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro   kwa mujibu wa sensa   ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti   vya kuzaliwa ni asilimi...

Fahamu Sifa za Mwanamke Asiyefaa Kuolewa Asilani .

Image
  SUALA la kuoa lipo tu licha ya kwamba wapo wanaochelewa kuingia kwenye maisha hayo wakihisi inaweza kusitisha furaha ya maisha yao. Nasema hivyo kwa kuwa najua wapo wanaoamini kuoa ama kuolewa ni kujiingiza kwenye matatizo. Dhana hiyo haina mashiko kiviile, asikuambie mtu unapoingia kwenye ndoa na mtu anayekupenda na wewe unampenda kwa dhati, karaha hakuna licha ya kwamba kugombana kwa hapa na pale hakuwezi kukosekana. Hata hivyo, nikiri tu kwamba, zipo ndoa ambazo ni ndoano. Yaani unakuta mtu kaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hakuwa amedhamiria, matokeo yake kadiri siku zinavyokwenda anahisi ameingia chaka na anaishia kuomba ndoa isiwepo. Leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao ni majanga na ukijichanganya ukaingia nao kwenye maisha ya ndoa, utakiona cha mtemakuni. 10. Asiyeridhika na penzi unalompa Wapo wanawake ambao wewe unaweza kujitahidi kumpatia mapenzi kadiri unavyoweza lakini yeye hatosheki. Anakuchukulia wewe ni dhaifu sana na wakati mwingine kuhisi yupo mwingine anaye...

Rapper AKA amwagana na mpenzi wake Bonang Matheba

Image
                         Rapper AKA ametangaza kupitia Twitter kuwa yeye na mtangazaji wa redio na TV, Bonang Matheba wameachana. Wawili hao walirejea kutoka kwenye mapumziko nchini Thailand wiki chache zilizopita na siku moja tu iliyopita walikuwa wakioneshana mahaba kwenye mitandao ya kijamii. “Sad to announce that myself and Bonang have broken up. We tried guys,” alitweet AKA. Hii ni mara ya pili AKA anatweet kuhusu kuachana na Bonang. Mwaka jana alisema hivyo pia lakini aliifuta post dakika chache baadaye, akisema kuwa waligombana na kisha kuachana. Bonang bado hajazungumza chochote kuhusu kuachana kwao. Katika msimu wa sikukuu mwishoni mwa mwaka jana, AKA alimkunisha Bonang na ndugu zake.

vyanzo 10 vya migogoro katika ndoa

Image
Ugomvi baina ya wapenzi katika mahusiano ni kitu cha kawaida kutokana na watu hao wawili kutoka katika malezi na mazingira tofauti ya ukuaji toka wakiwa wadogo hadi watu wazima. Wawili hao wanapoaanza kujenga mahusiano na kukaa pamoja kama familia,kuna vitu kadhaa ambavyo kila mmoja wao huvitazama tofauti na hivyo kuleta migongano. Migongano ambayo inaweza ikarekebishika kama wenza hao watamua kuifanyia kazi na kuelewana. Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano ndani ya mahusiano ya mke na mme na hapa tunaeleza sababu kuu ambazo kwa kawaida hutokea karibu katika kila mahususiano 1. Wivu Na Kukosa Kujiamini Wivu unatokana na jinsi ambavyo mpenzi mmoja anavyohusiana na watu wengine wa jinsia tofauti. Inaweza ikawa marafiki,wafanyakazi wenza au wapenzi wa zamani. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba wivu unasababisha ugomvi katika mahusiano mengi. Kunatakiwa kuweka mipaka ya kutosha na iliyo wazi ili kujenga uaminifu kwa mpenzi wako na kumpa kujiamini. Mpenzi ambaye hajiam...

Mambo 6 yatakayo kufanya ukose heshima kwenye jamii yako

Image
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa. Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu. Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda. Njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa. 1. Muonekano. Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani. Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dog...

Mambo 7 yanayowaumiza wanaume kwenye mahusiano

Image
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa. Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake. Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye kukimbiwa. Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama. Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa. Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wan...

Neno Gani Linaumiza Zaidi Kutoka Kwa Mpenzi Wako Unaempenda Kwa dhati Kati ya Haya:-

Image
  Neno Gani Linaumiza Zaidi Kutoka Kwa Mpenzi Wako Unaempenda Kwa dhati Kati ya Haya:- 1. Tuachane, 2. Sikutaki tena, 3. Nimepata mwngne, 4. Mbona king'ang'anizi wewe?, 5. Sikupendi, 6. Wazazi wangu hawakutaki, 7. Siwezi kuwa na wewe, 8. Kwako nilikosea njia tu, 9. Huna mvuto naona aibu, 10. Najuta kuwa na ww, 11. Huwezi kunihudumia fuata wajinga wenzio, 12. Wewe sio type yangu, 13. Dini zetu ni tofauti hivyo siwezi kuwa nawe... FUNGUKA HAPA MDAU mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin-top:0in; mso-para-margin-right:0in; mso-para-margin-bottom:10.0pt; mso-para-margin-left:0in; line-height:115%; mso-pagination:widow-orphan; font-size:11.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-ascii-font-family:Calibri; mso-ascii-theme-font:minor-latin; mso-fareast-font-family:"Times N...

MAMBO ya kuzingatia kabla ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi

Image
Mapenzi ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu anahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba. Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi. 1. ni lengo (ambition), kama ...

HIZI Ndio Sehemu 10 zenye Msisimko Mkali zaidi Kwenye Mwili wa Mwanamke

Image
  Kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo. Mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo  cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine. Kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo. 1. Kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa. Jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu. 2. Sikio; sikio ni sehemu yenye m...

FAHAMU Namna ya Kuishi na Mpenzi Anayependa Fedha...

Image
  HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana. Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha! Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana. Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.” Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiy...

MAPENZI yaoneshe kwa VITENDO nasio MANENO

Image
Kama ilivyo mambo mengine kuwa na ubunifu ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui. Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha  kwa kufuata haya mambo machache ambayo wanawake wengi huwa wanapenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na kivitendo. 1-Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara. 2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio). 3-Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi. 4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda ...

Dereva bodaboda akatwa sikio kwa tuhuma ya kufumaniwa na mke wa dereva teksi

Image
  Dereva bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara, amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na mke wa dereva wa teksi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Francis Massawe alisema tukio hilo lilitokea Desemba 21 saa 6:10 usiku kwenye Kitongoji cha Qendangonyi, Kata ya Ganana wilayani Hanang’. Kamanda Massawe alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na majeruhi amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa. Alisema wanamshikilia dereva teksi kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani. Source: Mwananchi

ROBOTI Inayoweza Kushiriki Ngono Kutengezwa

Image
  Hii teknolojia sasa imekuwa too much! Kila kukicha wenzetu wazungu wamekuwa wakibuni vitu vipya tofauti kabisa na fikira za kawaida za kibinadamu na kuendelea kuushangaza ulimwengu na viumbe vyake, hatujui tunaelekea wapi na hizi teknolojia zinazobuniwa na wenzetu kila siku. Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? Ungefunga ndoa na roboti? Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo? Haya ni baadhi ya maswali machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika Chuo Kikuu cha Goldsmith mjini London nchini Uingereza baada ya Serikali ya Malaysia ambayo ndio iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku. Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina na hapakuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo. Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono (roboti) ilidai kwamba itatengeza roboti wanaoweza kushiriki ngono na ...

USHAURI Kwa Kina Kaka: Unapoanza Mahusiano Mapya Epuka Wanawake wa Aina hii

Image
  1.MSICHANA WAKO WA ZAMANI Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni. 2.DADA WA RAFIKI YAKO KIPENZI Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgong...

Mambo yanayomfanya Mtu ayachukie Mapenzi.

Image
  DIANA NYANGE Sijui wewe ulikuwa una malengo gani wakati unafikiria kuwa na ambaye unaye; wapo ambao walikuwa na malengo kwamba akiwa na mwanaume, maana yake awe ndio sawa na mashine ya kutolewa fedha maarufu kama ATM. Ikiwa ulichokuwa unatafuta ni mwanaume au mwanamke ambaye kwako atakuwa ni ATM, kwamba ndiye awe anakupa kila kitu unachotaka, ikiwa hatakuwa na fedha si rahisi mkaendelea kuwa na uhusiano mzuri, kwa kuwa mpango wako haukuwa mapenzi, bali kuchuma fedha na kula raha. Wajinga ni wale ambao wanaingia kwenye mapenzi ili kusaidiwa tu, badala ya kusaidiana. Mwenye hekima ni yule ambaye anafahamu kwamba kuingia kwenye mapenzi, maana yake ni kuongeza timu ya kusaidiana katika maisha, si vinginevyo. Mwanamke yeyote ambaye anafikiri yuko na mwanaume maana yake ni kwamba awe anamnunulia kila kitu, kwamba kwake mwanaume ni kila kitu, kinywaji anunuliwe, chips anunuliwe nk…kwamba yeye ni mtu wa kupewa tu ofa, maana yake ni kwamba akili yake imekufa. Kufikiri kwamba kuoana na fu...