Posts

Showing posts with the label SIASA

Dr Slaa Ajitathimni Kurud Nchini.......Adai Upinzani Usipojipanga Unaweza Kufutika 2020

Image
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye kwa sasa anaishi nje ya nchi, Willbrod Slaa amesema anajitathmini kwa kile kilichomfanya aondoke hapa nchini na familia yake kama hakipo aweze kurejea nyumbani. Dkt. Slaa aliamua kuweka pembeni masuala ya siasa baada ya kutofautiana na chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea wa Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa. Amesema kuwa kwa sasa amemaliza masomo yake na baada ya kutafakari na kujitathmini atarejea nyumbani muda wowote. “Ni kweli nimemaliza masomo yangu, bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu, baada ya hapo nitaangalia uwezekano wa kurejea nyumbani,”amesema Dkt. Slaa. Aidha, kuhusu mwenendo mzima wa Serikali ya awamu ya Tano, amesema kuwa hakuna nchi hata moja ulimwenguni ambayo Rais wake atakubarika kwa asilimia mia moja, hivyo Rais Magufuli ameonyesha msimamo wa kusimamia kile anachokiamini Hata hivyo, ameongeza kuwa kama wapinzani hawat...

Makonda ahojiwa na kamati ya madaraka ya bunge

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge. Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.

Maalim Seif azipiga kufuli akaunti za CUF, Lipumba Alalamika

Image
  Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amelalamikia kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kuzifunga   akaunti zote za chama hicho za wilaya. Ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la uongozi linaloongozwa na upande wake. Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama kutoka serikalini wameikosa. “Wajumbe nawashukuru kwa kuja ili kupata fursa ya kujenga chama. Chama chetu kipo ndani ya mtihani ambao kwa kweli chanzo chake ni Katibu Mkuu wetu kutoheshimu katiba yetu na kutoheshimu taratibu za kidemokrasia,” amesema Prof. Lipumba. Aidha, Prof. Lipumba amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara. Magdalena Sakaaya. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga ku...

Alichokiandika Nape Nnauye Leo Kupitia Ukurasa wake wa Twitter

Image
Jana Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Nape Nnauye na nafasi yake akapewa Dr. Mwakyembe. Baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na waandishi wa habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano. Nape alilazimika kuzungumza akiwa juu ya gari lake.Hata hivyo, polisi waliingilia kati Leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa twitter, ametoa ujumbe kwa wanahabari nchini ambapo ameandika: "Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA!" Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA! pic.twitter.com/MjXwt3ZC0M — Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) March 24, 2017

Polisi Wazuia Mkutano wa Nape na Waandishi wa Habari......Alazimika Kuongea Akiwa Kwenye Gari Lake

Image
  Aliyekuwa Waziri wa Habari,   Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam   ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba uteuzi wake umetenguliwa. Hali hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuuzuia mkutano huo ambapo RPC Kinondoni alifunga barabara kwa gari kuzuia Gari ya Nape huku akiwataka waandishi wa habari watawanyike mara moja. ==> Haya ni machache ambayo Nape kayaongea 1.Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia. 2.Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. 3.Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. 4.Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa. 5.Niliikuta CCM iko shimoni nikaito...

Mbunge wa Nzega Hussein Bashe Afunguka Maneno Mazito Kuhusu Hali ya Kisiasa Ilivyo Hivi sasa Nchini

Image
Mbunge wa Nzega mjini kupitia CCM Hussein Bashe amepost ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno yaliyosomeka…"Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo "Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu. "Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru. "Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu. "Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu. "Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa taifa letu. TU...

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dkt. Kafumu na Makamu Vicky Kamata wajiuzulu sababu serikali inaingilia majukumu yao.

Image
  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao. Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo. Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye ofisi ya spika wa bunge jana.  

Lawrence Masha Ajitoa katika mbio za kugombea urais wa TLS .....Atangaza kumuunga mkono Tundu Lissu.

Image
                  Wakati kesho kukitarajiwa kufanyika uchaguzi wa Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika, leo wanasheria hao wamekuatana Arusha kwenye mkutano mkuu wa chama cha wanasheria hao. Katika mkutano huo,   aliyekuwa mgombea wa Urais wa TLS, Mwanasheria Lawrance Masha ametangaza kujiondoa kuwania Urais huo na   amesema anamuunga mkono Tundu Lissu na kura zake apigiwe Tundu Lissu.