Posts

Showing posts from February, 2017

Wasanii Wamkaanga Wema Sepetu.......Wakanusha Madai ya Kuidai CCM

Image
  Baadhi   ya wasanii wa kundi la Mama Ongea na Mwanao, waliokuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu, wamekanusha madai ya kutolipwa wala kukidai chama hicho madeni yoyote wakati na baada ya kampeni hizo kumalizika. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yusuph maarufu Batuli, alisema madai hayo si kweli kwani wasanii wote walilipwa na mikataba wanayo. “Nikiwa kama Makamu Mwenyekiti wa ‘group’ hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda, ni kweli kuna uvumi ulienea katika mitandao kwamba wasanii tulioshiriki kampeni na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu hatujalipwa, si kweli nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli. “Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais na kuichafua CCM, mimi nakataa, wasanii wote tulilipwa na mikataba ipo. "Haiwezekani wewe staa mkubwa ...

Mahakama Kuu Kuamua Dhamana ya Lema Ijumaa Hii.

Image
  Hatima ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), itajulikana Ijumaa wiki hii baada ya shauri hilo kurudishwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Hatua hiyo imekuja baafa ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kufuta rufaa mbili za Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), dhidi ya   mbunge huyo juzi mjini hapa. Mmoja wa mawakili anaomtetea mbunge huyo, Adam Jabir, alisema shauri hilo litaamuliwa Machi 3, mwaka huu mbele ya Jaji Salma Maghimbi kutokana na rufaa ya Jamhuri namba 135 ya mwaka jana, inayopinga uamuzi wa Novemba 11, mwaka jana wa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha kumpa Lema haki ya dhamana. Novemba 11 mwaka jana, Wakili Mwandamizi wa Serikali Paul Kadushi, alisimama wakati hakimu huyo akijiandaa kuandika masharti ya dhamana na kuieleza mahakama hiyo kuwa wameshasajili notisi ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu wakipinga uamuzi wa hakimu huyo kumpa Lema dhamana. Hata h...

Kimenukaa...Wabunge Wamlipua Steve Nyerere,Wakataa Kuombwa Msamaha..!!!

Image
                        Kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa mazungumzo ya mwigizaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu halijafutika, mengine yamefumka kwani baadhi ya wabunge waliotajwa kwenye sauti hiyo wamelimpua Steve. Mbali na wabunge kutajwa katika sauti hiyo iliyosambaa wiki iliyokatika, wasanii pia walitajwa ambao ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Romeo George ‘Rommy Jones’ na Ahmed Hashim ‘Petit Man’. Kwa upande wa wabunge ni Goodluck Millinga (CCM-Ulanga), Ahmed Shabiby (CCM-Gairo), Joseph Musukuma (CCMGeita Vijijini), Freeman Mbowe (Chadema-Hai) na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini). Steve pia aliwataja mawaziri wawili. Steve alisikika akiwataja wabunge hao akimwambia mama Wema kuwa, aliwafuata bungeni mjini Dodoma, Februari 6, mwaka huu ili wamsaidie bintiye aliposhakiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ kwa madai ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya ku...

Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu .

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote. Kauli hiyo ya Nape inakuja ikiwa ni takriban wiki tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aseme watu wanaotetea wale aliowataja hadharani kwa kuhusika na dawa za kulevya wengine ni wapenzi wao. “Wengine wanaumia tunagusa wapenzi wao, wawasaidie waache si kupiga kelele tu, ujumbe umefika,” alisema Makonda katika moja ya mikutano yake. Ingawa katika mkutano huo Makonda hakumtaja mtu kwa jina, lakini aliitoa kauli hiyo siku chache baada ya Nape kupinga mfumo wake wa kutaja majina ya watu hadharani, hususani wasanii na kuwatuhumu kuhusika na dawa za kulevya. Nape alisema kuwataja watu bila ushahidi ni kuwachafulia majina yao waliyoyatengeza kwa muda mrefu. Mbali na Nape, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM), alizungumza mara kadhaa bungeni akimpinga Makonda kwa mfumo wake aliokuwa akitumia, kutaj...

Adhabu za kikatili mashuleni zapigwa marufuku

Image
  Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kali na za kikatili kwa wanafunzi na badala yake waalimu wameelekezwa kutoa adhabu kulingana na taratibu na sheria zilizowekwa. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais katika uzinduzi wa ripoti ya elimu ya msingi nchini amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kinyume cha taratibu. Naye Mratibu wa Mtandao wa Elimu nchini ambao ni wasimamizi wa utafiti huo Bi. Cathrene Sekwao na mtafiti Bw. Jacob Kateri amesema wameamua kufanya utafiti huo ili kuweza kujua hali ya elimu ikoje ili serikali iweze kuona nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu ambapo pia wameitaka serikali kupitia mapendekezo yao.

Wafanyakazi wengine Wawili wa Quality Group ya Yusuf Manji Wafikishwa kizimbani.

Image
Wafanyakazi wengine wawili wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na Yusuf Manji ambao ni raia wa India wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kutimiza majukumu yao. Washitakiwa hao ni Jose Kiran (40) ambaye ni Meneja Miradi wa kampuni na Prakash Bhatt (35) ambaye ni Katibu Muhtasi wa kampuni hiyo ambao wameongezwa katika kesi inayowakabili wafanyakazi 14 wa kampuni hiyo, raia wa India wanaokabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kughushi viza ya biashara. Wakili wa Serikali, Method Kagoma alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu Namba 30 (1) (f) na Kifungu Namba 2 cha Sheria ya Uhamiaji ya Mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 8 ya Mwaka 2015. Kagoma alidai washitakiwa hao wawili, Februari 20 mwaka huu katika Kampuni ya Quality Group waliwazuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa ku...

Waziri Lukuvu Amnyang'anya Ardhi Makonda

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kumchukulia hatua mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Mohamed Iqbal aliyempa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda eneo la ukubwa wa ekari 1,500 ili kujenga viwanda vidogo, wakati linamilikiwa na serikali na si mali ya mfanyabiashara huyo. Jumanne iliyopita mfanyabiashara huyo alimkabidhi Makonda eneo la ukubwa wa ekari 1,500 Kigamboni, kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya wafanyabiashara. Ekari hizo zilitolewa na Kampuni ya Azimio Estate inayojihusisha na ujenzi wa majengo na uendelezaji wa ardhi na kukabidhiwa kwa Makonda. Kampuni hiyo pia iliwahi kutajwa katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu ushiriki wake katika miradi ya ujenzi wa nyumba za Shirika la Tafa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambao unadaiwa uligubikwa na ufisadi. Alipotembelea eneo hilo lililopo Kigamboni, Makonda aliipongeza kampuni hiyo kwa kukubali kutoa eneo lao na kusema wameonesha nia ya kuunga mkono juhudi za R...