Yanga imepoteza mchezo wa pili wa CAF dhidi ya TP Mazembe
June 28 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilirejea katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ndio uwanja inaoutumia kama uwanja wake wa nyumbani kucheza mechi yake ya pili hatua ya nane bora dhidi ya klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Katika mchezo huo wa Kundi A lenye timu za Medeama ya Ghana, Mo Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Kongo na Yanga, umemalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo limefungwa dakika ya 74 Merveille Bope, TP Mazembe walionekana kucheza kwa umakini na uzoefu mkubwa, kitu ambacho kimeisaidia kupata point tatu.
TEMBELEA SITE YETU KATIKA MICHEZO BARANI ULAYA ===>> BONYEZA HAPA
Comments
Post a Comment