Askari Aliyemuua Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Ahukumiwa Kifungo
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imetoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha Television cha chanel Ten, Daud Mwangosi.
Mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 mshtakiwa wa mauaji hayo, askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’ Pacificius Simon.
Hukumu hiyo imekuja baada ya juzi mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 2012 kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi wakatia CHADEMA ikifanya uzinduzi wa matawi, huku kukiwa na katazo la mikutano au makusanyiko ya kisiasa kutokana na seriakali kuongeza muda wa sensa ya watu na makazi
KAMA ULIKOSA HII TAARIFA BASI NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU, SHULE NNE ZA SEKONDARI NCHINI KENYA ZIMETEKETEA KWA MOTO, BONYEZA HAPA CHINI KUSOMA ZAIDI.
KAMA ULIKOSA HII TAARIFA BASI NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU, SHULE NNE ZA SEKONDARI NCHINI KENYA ZIMETEKETEA KWA MOTO, BONYEZA HAPA CHINI KUSOMA ZAIDI.
Comments
Post a Comment