Nape aipa tano kurugenzi mawasiliano Ikulu, habari maelezo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano. Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii. Akizungumza leo (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali. “Nawapongeza wakurugenzi vijana, Dk Hassan Abbasi (Maelezo) na Grayson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Seri...
Klabu ya Manchester United imesalia katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya wageni wao wa Bournemouth waliosalia na wachezaji 10 uwanjani. Mechi hiyo ilikumbwa na visa vya ukosefu wa nidhamu uliomuhusisha mshambuliaji wa United Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings wa Bournemouth. Visa vyote viwili vilitokea mwisho wa kipindi cha kwanza cha mechi baada ya wachezaji hao kuonywa na refa Kevin Friend. Alipewa kadi ya njano ambapo Friend aligundua ni yake ya pili na hivyobasi kutakiwa kutoka uwanjani. Marcos Rojo aliiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Bournemouth kusawazisha. Baadaye mshambuliaji wa United Ibrahimovic alishindwa kufunga mkwaju wa penalti baada ya beki wa Bournemouth kuunawa mpira langoni.
Mtoto wa kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa. => AJALI MBAYA YA BASI ILIYOTOKEA HII HAPA Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita. Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani alisema binti yake alitoweka nyumbani saa tano asubuhi, wakati wakiwa pamoja wakitazama televisheni. “Alitoka nje kama anaenda kucheza na wote hatukuwa na wasiwasi. Baada ya saa moja tulishtuka baada ya kutomuona, hivyo ikabidi tuanze kumtafuta,” alisema. Alisema walitoa taarifa polisi na kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio hadi jana mwili wake ulipokutwa umening’inizwa kwenye kisima cha nyumba ya jirani yao. “Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni kavu na ana majeraha,” alisema. ANGALIA AJALI MBAYA YA BASI =>BONYEZA HAPA Alisema kisima hicho kina tundu d...
Comments
Post a Comment