PREZZO AFUNGUKA JINSI UHUSIANO WAKE NA DIVA ULIVYOKUWA
Kumewahi kuwa na tetesi miaka ya nyuma kuwa msanii wa rap toka Kenya, Prezzo alikuwa anatoka kimapenzi na mtangazaji maarufu wa clouds FM,Diva kutokana na ukaribu waliokuwa nao mpaka kufikia hatua ya mtangazaji huyo kujichora tattoo yaPrezzo.
Alipoulizwa kuhusiana na tetesi hizo kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Prezzo alidai kuwa yeye na Diva zaidi ya kuwa washikaji hawajawai kujihusisha kwenye mambo ya mapenzi kama watu wengi wanavyodai.
“Mimi na Diva hatukuwahi ku date,tulikuwa washikaji.Sema bloggers wanaongeza chumvi kwa sababu tulikuwa close friends ila hatujawai ku date hata denda sijawahi kula bado” alifunguka Prezzo.
Alipoulizwa suala la mtangazaji huyo kujichora tattoo yake Prezzo alisema,”Alijichora tattoo si kwa vile mimi ni mshkaji wake,haimaanishi kulikuwa na kitu zaidi ya urafiki,kama ningekula vitu ningekula vitu ningesema tu sasa hivi“.
Moja ya picha iliyowahi kusambaa na kuchochea tetesi za wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi
Comments
Post a Comment