SAMIA- OLE WENU MAFISADI WA FEDHA ZA MIRADI


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano, itapambana kwa nguvu zote na vitendo vya ufisadi kwenye fedha, zinazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.


Amesema serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kudhibiti matumizi yasiyo lazima na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa, zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Alisema hayo jana wakati akifunga maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane kitaifa katika Uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa niaba ya Rais John Magufuli.

Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Makamu wa Rais alisema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia, iwapo tu vitendo vya ufisadi katika fedha zinazoelekezwa kwenye maendeleo utakoma.

Alisema pia hayo yatawezekana endapo wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati, kudai risiti, kufanya kazi kwa bidii na kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

Comments

Popular posts from this blog

MREMBO GIGY MONEY AFANYA KUFURU NYINGINE

Hamorapa kuhusu Ishu ya kumpigia Alikiba Magoti .