WAKAMATWA WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limekamata silaha moja ya kivita na risasi 122 zilizokutwa na watuhumiwa nane wakiwa na silaha nyingine za jadi walizo tumia kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Njombe na Iringa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protas akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa watuhumia hao walikutwa na silaha ya kivita yenye darubini aina ya long riffle, huku akizitaja silaha za jadi kuwa ni pamoja na shoka na nondo zinazodaiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya wizi.
Silaha ya aina hiyo inakamatwa ikiwa ni mara ya pili tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo silaha zote zimekamatwa wilaya ya kipolisi Makambako na watuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi wa jeshi hilo utakapo kamilika.
Aidha inadaiwa watuhumiwa hao walikutwa na dawa ya meno pamoja na mafuta ya kupaka.
CHANZO: MTEMBEZI.COM
Comments
Post a Comment