Popular posts from this blog
Diamond aingia kwenye biashara ya vipodozi, kuingiza sokini ‘ChibuPerfume’
Mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz ameonyesha sample yake ya kwanza ya bidhaa yake mpya ya perfume ‘ChibuPerfume’ inayotarajiwa kuingia sokoni siku za usoni. Muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa tayari kwa ajili ya ujio wa bidhaa hiyo ambayo itapatikana katika maduka mbalimbali ya vipodozi nchini. chanzo: BONGO5
Hamorapa kuhusu Ishu ya kumpigia Alikiba Magoti .
"Mi sijali watu watakaosema mimi ni team Kiba kwa kuwa niliamua kumpigia Alikiba magoti ile ilitokana na heshima na amefanya vitu vikubwa na kuwakilisha nchi yetu vizuri, kwa mimi namuhusudu saana Ali Kiba". Hayo ni Maneno ya Hamorapa Akiongea kupitia eNewz ya EATV, kuhusu maneno ya watu kuwa ameamua kujiweka upande wa Alikiba ingawa ameshindwa kujizuia kuonesha mahaba yake kwa msanii huyo. Harmorapa aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kufananishwa na msanii kutoka kundi la WCB Hamonize amesema hana mpango wa kubadilisha jina lake "labda iongezeke a.k.a tu" Hata hivyo Hamorapa amewapa ujumbe watu ambao wamamsema vibaya kwamba hawezi kuimba, wanapaswa kutambua kwamba wanavyomsema vibaya wanamfanya aongeze juhudi na kujua vingi kila siku kwa kutumia zile 'diss' wanazompa.
Comments
Post a Comment