Cristiano Ronaldo anarejea nyumbani Sporting Lisbon akiwa na kiatu maalum
Mchezaji Cristiano Ronaldo leo atavaa viatu maalum vyenye tarehe ya 8/6/2003 ikiwa na kumbukumbu ya siku maisha yake ya soka yalipobadilika baada ya kuichezea Sporting Lisbon katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester United.
Baada ya mechi hiyo, Man United wakiwa wamelala kwa mabao 3-1, Kocha Alex Ferguson alimueleza Ronaldo kwamba anamhitaji ajiunge na Man United.
Real Madrid itakuwa ugenii dimbani ikiivaa Sporting Lisbon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Cristiano Ronaldo atakuwa na furaha zaidi kwa kuwa atakuwa anarejea nyumbani tena, lakini safari hii akiwa na kiatu maalum.
Comments
Post a Comment