Dully Sykes adai umri na majukumu vilimfanya aipotezee bifu yake na TID
Alikuwa akizungumza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Alikiba na kudai kuwa ipo siku wakikua, wataacha.
“Hata mimi pia ilivyofikia kwenye age moja hivi nilikuwa na matatizo na TID, zamani. Lakini nilipoweza kukua niliacha hivyo, nilivyoanza kupata majukumu nikasahau kwamba tulikuwa na matatizo,” Dully alimweleza Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
Comments
Post a Comment