DHAMANI ya Mbunge Godbless Lema Yakwaa Kisiki Tena..Arudishwa Rumande

 
Mbunge Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo.

Rufaa hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.

Upande wa mtuhumiwa uliongezea muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda uliokuwa umepangwa awali.

Mbunge Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

Mtoto wa Miaka minne Auawa, Atupwa Kisimani

MOURINHO KUWAPIGA BEI WACHEZAJI 13 MAN UNITED

MWANAFUNZI Anusurika Kifo Baada ya Kukatwa Mapanga na Mwalimu