Maxence Melo Afunguka "Mtandao wa Jamii Forums Haujatetereka Bado Upo Ngangari"


Baada ya kuchiwa leo kwa dhamana Mwanzilishi mwenza wa JamiiForums, Maxence Melo amesema mtandao wa JamiiForums haujatetereka na bado uko ngangari na amewataka watumiaji wote wa mtandao huo waondoe hofu kwa kuwa taarifa zao za siri ziko salama.

Pia amesema hana ugomvi wowote na vyombo vya dola na ana imani na mahakama za hapa nchini kuwa zitamtendea haki katika kesi yake.

Amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kuendelea kupigania uhuru wa kusema na kutoa maoni, pia amevishukuru vyombo vyote vya habari na wanahabari kwa kumuunga mkono kipindi chote alipokuwa mahabusu.

Comments

Popular posts from this blog

Mtoto wa Miaka minne Auawa, Atupwa Kisimani

MOURINHO KUWAPIGA BEI WACHEZAJI 13 MAN UNITED

MWANAFUNZI Anusurika Kifo Baada ya Kukatwa Mapanga na Mwalimu