MKULIMA Aliyechomwa Mkuki na Wafugaji Apata Nafuu Baada ya Mkuki Kutolewa

 
Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa.

Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu.

Imetolewa na :- Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi

Comments

Popular posts from this blog

Mtoto wa Miaka minne Auawa, Atupwa Kisimani

MOURINHO KUWAPIGA BEI WACHEZAJI 13 MAN UNITED

MWANAFUNZI Anusurika Kifo Baada ya Kukatwa Mapanga na Mwalimu