MWAROBAINI wa EBOLA wapatikana.

Majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo na nguvu zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.
Majaribio yake yamefanywa nchini Guinea, mojawapo ya mataifa ya Afrika Magharibi ambayo yalikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambao ulimalizika mwaka huu.

Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yaliyochapishwa kwenye jarida la masuala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet, yanaonyesha kuwa takriban watu elfu sita waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.
Miongoni mwa kundi lingine kama hilo, ambao hawakupewa chanjo, watu 23 walipatikana na virusi vya Ebola.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi moja ya matibabu nchini Uingereza- Wellcome Trust, ameelezea matokeo hayo kama ya kufana mno.
Watu 11,000 walifariki wakati wa mlipuko wa hivi majuzi kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.
Comments
Post a Comment