RAIA 20 WAUWAWA KIKATILI MASHARIKI MWA DRC CONGO.

 Wapiganaji waasi wa ADF
Takriban raia 20 wameuawa katika mauaji ya kikatili katika jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kulinga na taarifa zilizotolewa na maafisa Jumapili.

Vifo hivi ni vya hivi karibuni katika wimbi la miaka miwili la ghasia katika jimbo hilo.

Mauji hayo yametokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na misururu ya mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700, kulingana na afisa katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu waasi kutoka Uganda kwa mashambulio ya hivi karibuni.

Maafisa wa Kongo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo , lakini ripoti kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi mengine, yakiwemo ya wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya mauaji.

Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa".

Teddy Kataliki, mkuu wa shirika maarufu la kiraia katika kanda hiyo, pia alisema kuwa waliouawa ni 22.

Lakini kasisi wa kikatoliki katika eneo hilo amesema kuwa waliouawa ni watu 27 na idadi inaweza kuongezeka zaidi " kama miili ya waliouawa itabainika katika msitu" unaopakana na mji huo.

Wakati mauaji ya kikatili ya Beni yalipofanyika Oktoba 2014, ADF walijibu haraka wakishutumu makundi mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na MONUSCO---Kikosi cha kulinda amani nchini DRC.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za kongo na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi linalotawala, huku serikali ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo na vita vya kidini vya Jihad.

Mauaji haya yanatokea huku mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya kutokana na hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula wake kumalizika taraehe 20 Disemba.

CHANZO: BBC swahili

Comments

Popular posts from this blog

Mtoto wa Miaka minne Auawa, Atupwa Kisimani

MOURINHO KUWAPIGA BEI WACHEZAJI 13 MAN UNITED

MWANAFUNZI Anusurika Kifo Baada ya Kukatwa Mapanga na Mwalimu