Federer amshinda Nadal kwenye Australian Open.

Roger Federer akisherehekea ushindi

Roger Federer amepata ushinda wa 18 wa Grand Slam kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano kwa kumshinda kwa seti tano mfululizo Rafael Nadal, katika fainali ya mashindano ya Australian Open.

Federer mwenye umri wa miaka 35 alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-1 3-6 6-3 na kupata ushindi wake wa tano wa Melbourne.

Nadal mwenye umri wa miaka 30 yuko nafasi ya pili sawa na Pete Sampras.
Ushindi mkubwa wa mwisho wa Federer ulikuwa wa Wimbledon mwaka 2012.


"Nimekuwa nikija hapa kwa karibu miaka 20 sasa,"alisema. Nimekuwa nikifarahia na sasa familia yangu inafurahia pia.

Federer akibusu kombe

Comments

Popular posts from this blog

MREMBO GIGY MONEY AFANYA KUFURU NYINGINE

Hamorapa kuhusu Ishu ya kumpigia Alikiba Magoti .