Jose Leonardo Ulloa agoma kuichezea Leicester City
Mchezaji wa klabu ya Leicester City Jose Leonardo Ulloa amegoma kuendelea kubakia katika klabu hiyo baada ya kuonyesha kukasirishwa na kocha wake Claudio Ranieri kukiuka makubaliano yao na kusema hawezi kuichezea tena Leicester sababu Ranieri kamsaliti.
Jose Leonardo Ulloa amesema kuwa Ranieri alisema angemruhusu kuondoka Leicester City na kwenda kujiunga na klabu nyingine endapo ingetoa ofa ya kuanzia pound milioni 4 na kuendelea, ila alishangazwa na kocha wake huyo hataki tena kuona nyota huyo akiondoka.
“Kocha wiki mbili zilizopita alisema kuwa kama ofa ya kati ya pound milioni 4 hadi 5 itakuja mezani ataniruhusu kuondoka lakini ninachokifahamu nikuwa ofa zilizokuja ni za kiwango hicho na zaidi lakini anazipotezea“
Hii ni Tweet ya Jose Leonardo kwa mashabiki wa Leicester City
Jose Leonardo Ulloa alijiunga na Leicester 2014, kaichezea jumla ya mechi 89 na kuifungia magoli 20.
Sunderland imeonesha nia ya kumuhitaji nyota huyo na ipo tayari kutoa pound milioni 7 kwa ajili yake, Sunderland wapo nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu ya Uengereza huku Leicester City wakiwa nafasi ya 15.
Comments
Post a Comment