Ni sawa rapper aliyedumu miaka 15 kushindanishwa na mwenye miaka 2 kwenye game? Haya ni maoni ya Mwana FA



Mwana FA anaamini kuwa katika muziki kushindanishwa kwa wasanii ni kitu ambacho hakiwezi kuepukika. Na katika miaka ya hivi karibuni ambapo shabiki ana access ya kukosoa, kusifia au kushindanisha, ndio imekuwa balaa kabisa, lakini hakukwepeki.

“Leo Mwana FA akitoa wimbo mzuri, watakuambia Mwana FA mkali kuliko fulani na fulani, kuna watu watakuambia MC fulani sababu ametoa wimbo sasa hivi, wimbo wake mkali basi MC fulani ndio mkubwa kuliko mamcee wote waliowahi kutokea nchi hii. Kama wanavyosema, opinion sio kitu ambacho mtu anaweza kushtakiwa kwa kuwa nacho, unless ni za kisiasa ama zina matatizo kwenye usalama wa taifa na vitu kama hivyo, lakini kila mtu anaruhusiwa kuwa na zake na hatuwezi kukulazimisha ubadilishe opinion zako,”

FA amesema tatizo pekee katika uhuru huo wa kujieleza na kuwa na majukwaa mengi ya kutoa maoni, watu ambao hawana uelewa wa kutosha katika kile wanachokielezea, hupotosha ukweli.

“Mfano halisi ni hili tunalolizungumzia, kuna watu hawajui muziki, wengine wameanza kusikiliza muziki miaka mitatu minne hii, au pengine wamesikiliza zamani, lakini wanausikiliza muziki juu juu, hawajui hata nini kinaendelea, wao wanaenda na hype tu, ngoma itakayohit ndio ngoma yao, msanii atakayehit ndio msanii bora kwa wakati huo. Kwahiyo watu wa aina hiyo wakitoa opinion zao unakuta msanii ana mwaka mmoja akalinganishwa na msanii ambaye ameweza kudumu kwenye game kwa miaka kumi na nne , kumi na tano na wakakuambia mwenye mwaka mmoja mzuri zaidi,” amesisitiza.

FA anasema kwa ukweli huo, wasanii hawapaswi kuumiza kichwa sana labda kama na watu ambao wanafahamika kuwa na uelewa mkubwa wa tasnia wakikumbwa na mafuriko ya hype.


“Haya maoni ya kwamba fulani ndio mcee mkali kuliko mamcee wote, yanatakiwa yaishie kuwa fulani ana wimbo mkali kuliko nyimbo zote za marapper zilizotoka kwa wakati huu. Msanii fulani ametoa wimbo mzuri kuliko nyimbo zote zilizotoka kwa wakati huu. Lakini hatumweki kwamba ndio msanii mzuri kuliko wote, ndio rapper bora kuliko wote kwa wakati huu, hiyo inakuwa disrespectful na inatakiwa isitiliwe uzito wowote. Ni kama yale maoni kwamba ‘huo wimbo wa FA wenyewe sijausikia lakini mbaya’, sasa hujausikia wimbo unakuaje mbaya?”

Comments

Popular posts from this blog

MREMBO GIGY MONEY AFANYA KUFURU NYINGINE

Hamorapa kuhusu Ishu ya kumpigia Alikiba Magoti .