Watu saba wahofiwa kufa maji Ziwa Tanganyika
Watu saba wanahofiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika baada ya boti ya MV Ngendo Buchuma waliyokuwa wakisafiria ikiwa na tani 20 za mzigo kutoka mjini Kigoma kwenda mji wa Kalemie Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Kongo kutoonekana kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji maboti Kigoma Uwamaki Edmud Kisinja amesema boti hiyo ikiwa na wafanyakazi wanne na wamiliki watatu wa mzigo wa vitunguu gunia 110,soda kreti 70,mafuta pipa 20 na ngano mifuko 180, waliondoka tarehe 23 mwezi wa kwanza lakini mpaka sasa hawajulikani walipo huku jitihada zikiwa zimefanywa kuwatafuta Mashariki ya DRC pamoja na upande wa Tanzania bila mafanikio hali inayoashiria huenda boti hiyo ambayo ilipaswa kutumia kati ya masaa 12 hadi 24 kufika DRC,imezama ziwani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma kamishna Msaidizi Mwandamizi Ferdinand Mtui amesema mpaka sasa hawajapata taarifa zozote kuhusiana na boti hiyo wala kuona mabaki ya mzigo wala miili ya watu na jitihada zinaendelea.
Comments
Post a Comment