Jarida la PEOPLE na TMZ wameripoti kuwa Beyonce na Jay Z wamepata watoto mapacha.
Tovuti ya TMZ imeripoti mapema leo kuwa Beyonce na Jay Z
wamepata watoto mapacha.
Hii imekuwa stori kubwa wiki nzima huku mashabiki wakisubiri
lini Beyonce atajifungua. Watoto hao wawili wa The Carters wamezaliwa kwenye
hospitali mjini Los Angeles.
Mpaka sasa haijulikani jinsia za watoto hao, palikuwa na
tetesi ni mvulana na msichana, ila hakuna ushahidi tosha wa kupitisha hilo…
Jay Z na Beyonce tayari wana mtoto wa miaka mitano, Blue Ivy
Comments
Post a Comment