Mimi Mars Amkana Dada Ake Vanessa Mdee
Msanii anayechipukia kutoka 'Mdee Music' Mimi mars
amefunguka na kuweka wazi kwamba hataweza kushirikiana na dada yake Vanessa
Mdee katika kuandaa kazi ya pamoja kwa kipindi hiki kwa sababu ya mashabiki
zake bado wanashindwa kutofautisha sauti zao
Mars ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya unaokwenda kwa
jina la 'Dedee' amesema kwa sasa yupo kwe wakati mgumu wa kujitofautisha na
dada yake huyo kwai sauti zao zimekuwa zikiwachanganya mashabiki zao kiasi cha
kuonekana kama Vanessa.
Akizungumza na eNewz ya EATV Mars amesema kwamba
"Mission yangu ni kujitahidi kubadilisha suala la kufanana na Vanessa,
kwani mashabiki na watu wengine wamekuwa wakisema tunafanana uimbaji . Nadhani
kwa sababu bado ni mapema hawajazoea kwani mimi ni mgeni lakini
niyahakikisha nakuwa tofauti ila ikishindikana kubadilika,
nadhani watakuwa wameshazoea na hata kututofautisha wao wenyewe. Lakini niwe mkweli
Vanessa siwezi kufanya naye kazi sahivi mpaka watu waweze kututofautisha ili
isije ikaonekana yeye ndo kaimba wimbo wote peke yake, pia hatuwezi kuunda
kundi moja la muziki bali tutaendelea kusaidiana na kuachia kazi huko mbeleni"- Mimi Mars.
Comments
Post a Comment