Picha ya Utupu ya Amber Rose Yafutwa..!!!
Mtandao wa kijamii wa Instagram wenye watumiaji zaidi ya
milioni 500 duniani umefuta picha ya utupu ya mwanamitindo Amber Rose.
Picha hiyo ambayo Amber aliiweka kwenye mtandao huo,
ilifutwa kutokana na kukosa maadili. Mara nyingi mtandao huo huziondoa picha
ambazo zinaripotiwa kutokuwa na maadili.
Baada ya kufutwa picha hiyo ya utupu ambayo imewatoa udenda
vidume wengi mitandaoni, Amber ameandika ujumbe mwingine kwenye mtandao huo
unaoonyesha masikitiko yake baada ya kufutiwa picha hiyo huku mashabiki
wakimuunga mkono kwa kitendo hicho.
Comments
Post a Comment