Picha za Beckham Akiwa Mbugani Zawatoa Mapovu Wasanii wa Bongo..Lulu Amvaa Kichwakichwa Bila Kujielewa..!!

David Beckham anaonekana kuwachanganya baadhi ya watu kwa
kitendo chake cha kupost picha mitandaoni bila kutaja kama yupo katika moja ya
mbuga hapa nchini Tanzania.
Beckham alitua nchini kimya kimya wikiendi iliyopita majira
ya usiku akiwa ameongozana na familia yake na kuelekea mahali pasipo julikana
huku baadhi ya wadau wakidai alikuwa ameelekea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.
Kitendo hiko kimewafanya watu kumshambulia kwenye kila picha
aliyopost mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza.
Hata baadhi ya mastaa wa Bongo wameonekana kushangazwa na
kitendo hicho huku wengine wakitoa yao ya moyoni kupitia mtandao wa Twitter,
kati yao ni Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Mwasiti. “Mbona hatoi Taarifa kwa wenye
nchi Yetu🤣🤣🤣🤣atajuta
nipe username yake kwanza 🤣🤣🤣🤣hata
simfologi,” ameandika Lulu.
Naye Mwasiti ameandika, “😂😂
huyu beckham huyu..sasa sisi ni mwendo wa kuweka bendera yetu 🇹🇿🇹🇿 tu kwenye kila picha yake
mbugani kagoma kusema alipo 😂😂@OfficialLizyM.”
Hata hivyo Fid Q amewachana watu wanaolalamikia tukio hilo,
“Nimekuta watu wananung’unika juu ya suala zima la ujio wa DEVI mbugani kwetu
eti kwasababu kila akipost hasemi kama yupo TZ..Mlimfadhili? 😀.”
Comments
Post a Comment