MWANAMUZIKI Chid Benz Amshushia Mkwala Mzito Chin Bees...
Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amemtaka msanii mwenzake
Chin Bees kutafuta jina lingine.
Sababu ya Chid Benz kusema hivyo imetokana na majina yao
kufanana, na kuongeza kuwa wote wanafanya muziki wa aina tofauti hivyo kulikuwa
hakuna ulazima wa ufanya hivyo.
“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza
huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani,
akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya
yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia
kwenye stage nachapa tu,” Chid Benz ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na
kuhoji.
“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina
lingine,” amemaliza kwa kusema.
Comments
Post a Comment