SHETTA Amchana Diamond Kiaina Kuhusu Kutoa Nyimbo Mfululizo.....
Msanii wa Bongo Flava, Shetta amesema haamini kutoa nyimbo
nyingi kwa wakati mmoja ni sababu ya kufanya vizuri.
Shetta ambaye amekaa kipindi kirefu bila kutoa ngoma,
ameiambia EA Radio kuwa yeye anaamini katika kujipanga zaidi na kutoa ngoma
kali.
“Mimi siamini kwenye kutoa nyimbo nyingi ndio ku-trend,
nafikiri kujipanga kwangu ndio huwa kuna sababisha kukaa muda mrefu bila kutoa
wimbo, ningekuwa naweza kujipanga haraka ningeweza kutoa madude haraka lakini
so far so good ngoja tutaibadilisha, ngoja tuone system yetu tufaifanyaje,”
amesema Shetta.
Ameongeza kuwa, “naamini ukitoa kazi ambayo umejipanga nayo
watu wanaweza wakaenyoy mwaka mzima au miaka miwili, kukaa kimya haijawahi
kunihadhiri kwa chochote sana sana watu wananimisi lakini ninapokuja watu
wanakuwa wananipokea, so am happy katika kitu ninachokifanya,” amesisitiza.
Comments
Post a Comment