Posts

Showing posts from May, 2016

Msichana wa Kazi za Ndani Afikishwa Mahakani Kwa Kuua Mtoto Mchanga

Image
NAIROBI, KENYA: Msichana wa kazi za ndani mwenye miaka 20 afikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mchanga wa miezi nane. WAKIMBIZI NCHINI NIGERIA WAKIMBILIA VISIWA VYA MEDITERANIAN HABARI KAMILI >>   BONYEZA HAPA CHANZO: UDAKU SPECIAL

Amboni Tanga: Watu 8 Wauawa kwa Kufichua vitendo vya Kihalifu

Image
Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo. Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo. BONYEZA HAPA   >> REAL MADRID YAZIDI KUTABA BARANI ULAYA Chanzo : Radio One.

Diva Azungumzia Mabusu yake na GK Yaliyozua Mjadala Mtandaoni

Image
Diva the Bawse anasema hataki kusikia kitu kinachoitwa ‘mila na desturi’ za Mtanzania hasa pale anapofanya kitu kinachompa furaha. Wiki hii mtangazaji huyo wa Clouds FM amesababisha mjadala mkubwa kwenye Instagram baada ya kupost video inayomuonesha akipigana French kiss na mpenzi wake rapper GK. “Trying kanye west n kim k yummy tongie crazyyy kiss… guess what. wedding very soon #theregoesmybabyyyyy,” aliandika kwenye video hiyo. “Nataka niishi the life that I want, mimi I don’t live to please anyone. I just live me as Diva, I just want to be happy,” Diva ameiambia Bongo5. “The kiss to happiness – tongue kiss is the key to happiness ndio maana mimi sioni ajabu kumkiss mtu.” Mtazame Hapa: 

Ukweli wa taarifa za Kipre Tchetche kusaini Oman, umeelezwa na C.E.O wa Azam FC

Image
Baada ya kuenea kwa habari za mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Azam FC Kipre Tchetche kuripotiwa kusaini klabu ya Nahda Al-Buraimi ya Oman, afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ameeleza ukweli na kuwatoa hofu mashabiki walioshtushwa na habari hizo. C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba kaeleza kuwa hizo ni habari za uzushi za kuwa nyota wao amesaini Nahda Al-Buraimi ya Oman, kwani bado ana mkataba na Azam FC ndio maana hata vyombo vya habari vinaripoti kuwa anaomba akapate changamoto mpya kwa maana ana mkataba na Azam FC. “Kipre ni mchezaji wetu ambae ni muhimu huwezi kumruhusu amalize msimu aende mapumziko akiwa hana mkataba, kwa hiyo tuna mkataba ambao ni endelevu, nadhani ndio maana ukasikia wanasema anaomba akapate changamoto sehemu nyingine, ukweli ni kuwa mchezaji kama ana mkataba ni makubaliano umuuze au anunue mkataba”

Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe

Image
MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani. Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo. Anayetuhumiwa kuua mumewe Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori amekiri kuhusika. Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliamua kum...

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Profesa Tunus Mgaya Aliyesimamishwa Kazi na Waziri wa Elimu Afunguka Mambo Mazito

Image
ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa. Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao. “Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi. Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa m...

Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa!

Image
Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne. Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January. SOMA HAPA   >>Serikali ya Nigeria yaingia matatani Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya…… ’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’ ’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa k...

Magazeti ya Tanzania yameamka na hizi leo May 31, 2016 kwenye, Udaku, na michezo

Image
Magazeti ya Tanzania yameamka na hizi leo May 31, 2016 kwenye, Udaku, na michezo

Wanawake Kenya Waandamana Kudai Waume zao Wanashindwa Kuwapa Mimba

Image
Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume. Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Akhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi. SOMA HAPA >>  REAL MADRID YAZUA GUMZO ZITO BAADA YA KUTWAA UBINGWA BARANI ULAYA Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji  hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa. Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao

Ndani ya siku 20 tu, Mabasi 34 ya DART, yashapata ajali

Image
Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART. SOMA HAPA   >> BOKO HARAM WATEKA WANAFUNZI NA KUWALAWITI HUKO NIGERIA

UKAWA yatangaza Kutokuwa na Imani na Naibu Spika

Image
UKAWA yatangaza kutokuwa na Imani na spika, Inaandaa mchakato wa kupiga kura ya kumuondoa madarakani. Yatangaza kususia vikao vyote atakavyo visimamia Habari kamili Kufuata hivi punde!!

Wema Sepetu Akubali Ndoa na Idris, Asema haya Kuhusu Ndoa yao itavyokua

Image
Penzi la Wema na Idriss kwa sasa linazidi kupamba moto, mpaka kupelekea Wema Sepetu kuanza kuwaza kufunga ndoa na Idriss. Wema alifunguka hayo katika video alipoulizwa na shabiki yake ni lini atafunga ndoa na Idriss. Na Wema

Hoja ya Dharura Wanachuo 7000 UDOM: Naibu Spika Aahirisha Bunge Baada ya Wabunge Kwa Pamoja Kutoka nje

Image
Bunge limechafuka muda huu baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kuomba mwongozo wa kujadili hoja ya wanafunzi zaidi ya 700 waliofukuzwa chuoni ijadiliwe kama hoja ya dharura. Naibu spika akaendeleza ubabe hivyo wabunge wa vyama vyote walisimama na kutoka nje.

Sasa Hivi Jackline Wolper Anamuita Diamond Platnumz Jina Hili Hapa

Image
Katika mahojiano na Take One ya Clouds TV  na Zamaradi Mketema, Jackline Wolper ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na penzi lake la Harmonize, Diamond ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake anachukuliaje mahusiano yao? “Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamondi ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu, “kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”

Gabo Zigamba Asema "Mimi Ni Zaidi Ya Ray, Naweza Kufanya Kitu Zaidi Yake"

Image
Msanii wa filamu nchini ambaye anafahamika kwa kuigiza kwa lafudhi ya Kimakonde Gambo Zigamba amefunguka na kusema kuwa yeye ni zaidi ya msanii Ray Kigosi kwenye kazi kwani yeye anafanya zaidi ya Ray. Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Gambo Zigamba aliweka wazi kuwa kipindi ambacho wakina Ray na wasanii wengine wakongwe wanafanya kazi zao hizo kulikuwa hakuna wasanii wengine wachanga ndiyo maana walikuwa wanaonekani ni wazuri sana lakini hivi sasa tasnia imekuwa na vipaji vipya ambavyo vinafanya vizuri zaidi yao hao wakongwe. Mbali na hilo msanii huyo alikubali kuwa msanii Ray Kigosi ana ladha zake katika kazi na ana mashabiki wake katika tasnia hiyo ila anachoamini yeye ni zaidi ya Ray Kigosi na kusema wapo watu wana uwezo wa kufanya kitu zaidi ya huyo Ray. "Ray ana flavor (ladha) zake na wapo watu wapo wanampenda Ray lakini kuna watu zaidi ya Ray wanaweza kufanya vizuri zaidi ya Ray, ila naweza kusema mimi ni zaidi ya Ray kwani naweza kufanya kitu zaidi ya Ray, Ray akabaki am...

PICHA: Jose Mourinho amesaini Man United, taarifa rasmi kutoka Sky Sport

Image
Huenda huu ndio ukawa mwisho wa headlines za Jose Mourinho kuhusishwa kujiunga na klabu ya Man United, kwani taarifa kutoka mitandao mingi ya soka Ulaya ikiwemo Sky Sport unaripoti kocha huyo kujiunga na Man United. Sky Sport wameripoti Jose Mourinho kusaini mkataba rasmi na Man United, kinachosubiriwa ni uongozi wa klabu hiyo kumtangaza tu, kwani leo May 26 ameonekana katika hoteli London akiripotiwa kuwa alikuwa na kikao na mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 20, Ikiwemo ya Magufuli Kutokuwa na Rafiki

Image
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo  May 20, Ikiwemo ya Magufuli Kutokuwa na Rafiki