Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. PILIPILI Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya...