Posts

Showing posts from November, 2016

NIMEFANYA Video Karibia 10 Lakini ya Diamond Mnaniuliza Kila Saa, Who is Diamond Motherf**** – Tunda

Image
Tunda amechoka kuulizwa maswali kuhusiana na kuonekana kwenye video ya Diamond ya wimbo Salome aliomshirikisha Ray Vanny. Ni kwasababu anajiuliza, iweje ameshaonekana kwenye video takriban 10, lakini tangu aonekane kwenye video ya Diamond, swali limekuwa lile lile na ni kama vile watu ndio wameanza kumuonea kupitia video hiyo. Kutokana na kuchoshwa na swali hilo, Tunda anayedaiwa kurudiana na mpenzi wake Young Dee, amempa jibu kavu mtangazaji wa Jembe FM, Natty E aliyemrushia swali lile lile limkeralo. “Nimefanya video ngapi? Nimefanya video karibia 10 lakini hii ya Diamond mnanifanyia interview kila saa,” Tunda alimjibu Natty. “Diamond, Diamond, who is Diamond motherf*cker. Weka hiyo kwenye gazeti lako,” aliongeza. Natty alijikaza na kumjibu ‘Anyway, Unaweza acha hilo swali la kuhusu Diamond, it’s not a big deal.’ Tunda alijibu kikauzu zaidi, “Maswali yote jibu lake ndio hilo.” Anachoshindwa kukielewa Tunda ni kuwa kushiriki kwenye Salome ya Diamond ni hatua kubwa zaidi katika ca...

SCORPION Akana Hoja 6, Akiri Hoja 3 Ikiwemo Kupata Mafunzo ya Kareti

Image
  MSHITAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete (34) ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya kareti kutoka chuo cha mafunzo cha Ifakara aliyoyafanya mwaka 1989 hadi 1995. Aidha, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umemuongezea mashitaka ya shambulio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashitaka. Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali ambapo katika maelezo ya zaidi ya saa nane, alikiri kuhusu jina lake, sehemu anayoishi ya Machimbo Yombo na mafunzo hayo. Hata hivyo, alikana kuhusu jina la Scorpion, mashitaka yake na kwamba hakukamatwa wala kuhojiwa na Polisi kuhusu mashitaka hayo. Katuga alidai kuwa Septemba 6, mwaka huu, mshitakiwa alikuwa maeneo ya Buguruni Sheli na kwamba Septemba 12, alihojiwa na kukamatwa na polisi maelezo ambayo aliyakana. “Mashahidi watakaotoa ushahi...

BAADA ya Weusi Kuwa na Kigugumizi Kuhusu Lord Eyes..Baraka The Prince Aamua Kumchukua Kwenye Lebo yake

Image
Na mwimbaji wa bongofleva Baraka The Prince ameingia kwenye headlines za kusimamia wasanii na sasa kaanzisha Label iitwayo BANA itakayosimamiwa na watu wawili ambao ni Baraka na mpenzi wake Naj. BANA tayari imeshafanya mazungumzo na kujiweka kwenye mstari wa kufanya kazi kwa kuwasimamia Wasanii watatu akiwemo Rapper Lord Eyes

Lady Jaydee aijibu kauli ya Ruge kuhusu Clouds FM kuwa tayari kucheza nyimbo zake

Image
   Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake. “Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ??😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️ #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide. Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL. “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tu...

RUGE Awachana Basata...Adai Wamekuwa Kama Polisi Badala ya Kuendeleza Sanaa Tanzania

Image
  Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA linapaswa kubadili mfumo wa ufanyaji kazi kwakuwa kwa sasa linafanya kazi kama polisi kuliko kuuendeleza muziki wa Tanzania. Akiongea kwenye kipindi cha XXL Ijumaa hii, Ruge alisema baraza hilo limekuwa likionekana zaidi katika kuwaadhibu au kuwafungia wasanii kuliko kusaidia kukua kwa muziki ikiwemo kutoa milango zaidi kwa watu wanaotaka kuanzisha tuzo. “Mlolongo wa tuzo unakuwa ni mgumu wakati ni jambo ambalo linatakiwa kupewa msukumo mkubwa sana. Baraza la sanaa, na vyombo vingine vimekuwa vikifanya zaidi ya upolisi kuliko kusukuma,” alisema. Amedai kuwa kutokana na BASATA kupenda kufungia video au nyimbo, wasanii wamekuwa wakifanya makusudi kwakuwa kazi zao hupata kiki na video zao Youtube kupata views zaidi zinazowapa fedha kuliko kazi kuchezwa kwenye TV. Anaamini kuwa baraza hilo linapaswa kuwa mbele kiteknolojia na kimawazo kuliko hata wasanii wen...

Rais wa Zamani wa Cuba, Fidel Castro Afariki Dunia

Image
  Rais wa zamani wa Cuba na kiongozi wa mapinduzi ya kikomunisti, Fidel Castro amefariki akiwa na umri wa miaka 90, mdogo wake Raul ametangaza. Amefariki usiku wa saa nne na dakika 22, kwa mujibu wa Rais Raul Castro. Fidel Castro aliiongoza Cuba kama nchi ya chama kimoja kwa takriban miaka 50 kabla ya Raul kushika madaraka mwaka 2008. Mazishi yake yanafanyika Jumamosi hii kwa mwili wake kuchomwa moto. Kutakuwepo na siku kadhaa za maombolezo ya nchi nzima.

Mwana FA Alaani Bifu za Wasanii Zinazoelea..Adai Busara Inahitajika la Sivyo Watatoana Macho

Image
  Mwana FA ameonya kuhusu bifu zinazoendelea kwenye muziki wa Bongo Flava kwamba zinakoelekea, watu wanaweza kufanyiana vitu vya hatari zaidi. Akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV jana, FA amesema busara zinahitajika kumaliza tofauti baina ya wasanii wanaohusika kwenye bifu hizo. . “Tufike mahali kwamba tujiwekee mipaka kama binadamu kwamba hivi vitu ambavyo tunaambiana kama ungekuwa unaambiwa wewe na familia yako ingekuwa sawa? Maana yake tunavyoelekea tutatoana macho hivi karibuni,” alisema rapper huyo. . “Watu pekee wanaoweza kufanya ni wao wenyewe wanaohusika. Nafikiri watu wawe humble, warudi chini kidogo, wanaelea sana juu, turudi chini kidogo, tujikumbuke sisi nani na kama malengo yetu ni kutoana roho ama kuendelea kufanya muziki tuweze kujitengenezea vipato,” amesisitiza. Ushauri wa Mwanafa umekuja katika wakati ambao uhasama kati ya kambi ya Diamond na Alikiba unazidi kushika kasi. Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake mpya #DumeSuruali aliyomshirikis...

Neymar kwenda jela miaka miwili

Image
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar, anatakiwa kupata kifungo cha miaka miwili hii ni baada ya waendesha mashtaka wa nchini Uhispania kudai kuhusika kwake katika kesi ya ufisadi kuhusu uhamisho wake kutoka klabu ya Santos nchini Brazil mwaka 2013. Jaji Jose Perals pia ametaka aliyekuwa rais wa Barcelona sandro Rosell kwenda jela kwa miaka mitano mbali na kupigwa faini ya Yuro milioni 7.2 kwa klabu hiyo. Imetaka kutupiliwa mbali kwa mashtaka dhidi ya rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria bartomeu. Rosell,Neymar na babake wanatarajwa kushtakiwa. Kesi hiyo inatokana na malalamishi ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS ,ambalo linamiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar na linadai lilipata fedha chache ikilinganishwa na zile lililotarajia. Aliyekuwa rais wa Barcelona, Rosell alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mwaka 2014 kwa jukumu lake katika uhamisho huo na kutoa ushahidi mahakamani mnamo mwezi Februari pamoja na Bartomeu,Neymar na babake Neymar. Chanzo: Bongo5.com

Mchungaji Atumia Dawa ya Mbu ya Doom Kuwaponesha Watu Kwa Miujiza

Image
Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali. Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, mchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi. Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko. Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu. Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba. Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo ,anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake. Amemue...

Jeshi la Polisi lakamata watumiaji wa shisha Dar

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na oparesheni juu ya matumizi ya shisha huku watu watatu wa wilaya Kinondoni wakishikiliwa kwa matumizi ya madawa hayo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro amesema amepokea taarifa hizo kutoka kwa RPC wa Kinondoni kuwa amepokea taarifa hizo na vielelezo vipo. “Oparesheni dhidi ya shisha bado inaendelea na leo RPC wa Kinondoni ameniambia wamekamata watu wa watatu na vielelezo kwahiyo vile vielelezo kwa kawaida vitapelekwa kwa mkemia wa serikali taratibu zitafanyika na watapelekwa mahakamani,”alisema Kamanda Sirro. Aidha Kamanda Sirro amewaomba wananchi kupinga utumizi wa madawa hayo huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

Dela adai amekuwa kama mwalimu wa Kiswahili baada ya cover ya Hello

Image
Muimbaji wa Kenya Adeline Maranga aka Dela aliyewahi kufanya cover ya wimbo wa ‘Hello’ wa Adele amesema kuimba kwa Kiswahili kwenye wimbo huo kumemuongezea umaarufu zaidi na sasa amekuwa kama mwalimu wa lugha hiyo. Dela amemuambia mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa amepata comment nyingi kutoka kwa mashabiki ambao wengi wanatamani kujifunza Kiswahili baada ya kuusikia wimbo huo. “Kuna watu hata ukiangalia comment zao kwenye Youtube wanasema kwamba hawajui Kiswahili lakini sasa wanataka kujifunza Kiswahili au wanasema mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili hapa America na nitawaimbia wanafunzi wenzangu huu wimbo. Pia na mimi nimekuwa mwalimu kwa njia ya Kiswahili,” amesema Dela.

Cristiano Ronaldo anarejea nyumbani Sporting Lisbon akiwa na kiatu maalum

Image
Mchezaji Cristiano Ronaldo leo atavaa viatu maalum vyenye tarehe ya 8/6/2003 ikiwa na kumbukumbu ya siku maisha yake ya soka yalipobadilika baada ya kuichezea Sporting Lisbon katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester United. Baada ya mechi hiyo, Man United wakiwa wamelala kwa mabao 3-1, Kocha Alex Ferguson alimueleza Ronaldo kwamba anamhitaji ajiunge na Man United. Real Madrid itakuwa ugenii dimbani ikiivaa Sporting Lisbon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Cristiano Ronaldo atakuwa na furaha zaidi kwa kuwa atakuwa anarejea nyumbani tena, lakini safari hii akiwa na kiatu maalum.

Taarifa:Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Ujumbe Wake Hawakuzuiwa Kusafiri Uwanja wa Ndege Dar es Salaam

Image
  Jana Asubuhi iliandikwa Habari iliyokuwa imechapishwa kwenye gazeti la Tanzania la kila siku ‘Mtanzania’ ambapo kichwa cha habari cha taarifa hiyo kilikuwa kikisomeka ‘Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete azuiwa kusafiri nje ya nchi uwanja wa ndege Dar es Salaam.’ Katika habari hiyo, gazeti hilo liliandika kuwa kutokana na taarifa lililozipokea ni kuwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete na ujumbe waka jana walishindwa kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Abudhabi kupitia Dubai baada ya mmoja wa wajumbe aliokuwa ameambatana nao kutokuwa na viza ya kusafiria wakati wa ukaguzi. Aidha, taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa hata baada ya mjumbe huyo kupata viza yake nusu saa kabla ya safari kuanza, walishindwa kuendelea kwani zoezi la ukaguzi wa abiria wanaosafiri na ndege hiyo lilikuwa limekwisha fungwa na ndege ikaondoka. Kutokana na hali hiyo, gazeti hilo lilieleza kuwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete aliyekuwa ameambatana na mkewe pamoja na wajumbe wengine wan...

Mwanamke Afa Akiombewa Kwa ‘Nabii’, Akutwa Hana Nywele Kichwani Pamoja na Nyusi za Macho

Image
  Mwanamke mkazi wa Unga-Limited jijini hapa, Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini hapa. Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na mumewe aliyemtambulisha kama Shafii Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa ‘Mtume,’ huyo. “Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo. Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia ‘huduma,’ hiyo. Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo wakiongeza kuwa tayari watu wawili wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha ‘ma...

Kinara wa Matusi Instagram Akamatwa na Polisi Baada ya Kutoa Matusi Makubwa Kuhusu Perfume Mpya ya Diamond

Image
Kijana mmoja ambaye anatumia jina la Shilolekiuno_official Huko Instagram  hatimae amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutukana na kukashifu watu mbali mbali mtandaoni, kijana huyo amekuwa akiandika matusi mazito na kukashifu watu mbalimbali akiwemo Mwanamuziki Diamond,  Jana Baada ya Diamond Kutangaza Kuleta Perfume mpya zenye jina lake sokoni, mtu huyo anayetumua jina la @shilolekiuno_officail aliingia mtandaoni na kuandika matusi makubwa ambayo siwezi kuyaweka hapa kuhusu Perfume hiyo ya Diamond Lemutuz Naye Ameandika Haya:

Carrick adai anatamani kubaki Man United lakini huu unaweza ukawa msimu wake wa mwisho

Image
Mchezaji wa klabu ya Manchester united, Michael Carrick ambae hadi saivi ameshacheza zaidi ya mechi 300 amesema inabidi awe mkweli kuhusu future yake ndani ya United. Carrick saivi anamiaka 35 anaona muda wake wa kuendelea kubaki Old Trafford umefika mwisho pia kutoka na kuja kwa Paul Pogba. Carrick wakatai anaongea na Sky Sport alisema, “Hii ni club kubwa na ninafuraha sana kucheza hapa kwa muda mrefu. Sasa hivi nina miaka 35 na inabidi niwe mkweli juu yangu hapa kwenye club japokua sitaweza kutabiri nini kitatokea msimu ujao.” Hadi saivi kocha Mourinho chaguo lake kubwa amekuwa mchezaji Paul Pogba ambae amesajiliwa kwa gharama kubwa zaidi.

Diamond aingia kwenye biashara ya vipodozi, kuingiza sokini ‘ChibuPerfume’

Image
  Mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz ameonyesha sample yake ya kwanza ya bidhaa yake mpya ya perfume ‘ChibuPerfume’ inayotarajiwa kuingia sokoni siku za usoni. Muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa tayari kwa ajili ya ujio wa bidhaa hiyo ambayo itapatikana katika maduka mbalimbali ya vipodozi nchini. chanzo: BONGO5

Waziri Mkuu kumtumbua Makonda iwapo atashindwa kukomesha matumizi ya shisha

Image
   Warizi Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha. Hatua hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga lakini akakataa. Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam. Alisema katika udhibiti wa suala la shisha, mkuu huyo wa mkoa amefanya kazi nzuri, na kwamba kwa kuwa ameshatoa maelekezo, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Makonda hana budi kuyatekeleza. Alisema alivyosikia anawaagiza wakuu wake wa wilaya wote kusimamia maagizo yake na kama hawakusimamia atachukua hatua, basi naye ...

Guardiola huwakataza wachezaji kufanya mapenzi baada ya saa 6 usiku – Nasri

Image
Mchezaji wa Ufaransa katika safu ya kati Samir Nasri amefichua kwamba mojawapo ya ufanisi mkubwa wa mkufunzi Manchester City Pep Guradiola ni kuwaagiza wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya saa sita usiku. Katika mahojiano na runinga ya Ufaransa, Nasri amesema kuwa Guardiola aliweka sheria hiyo hata iwapo kungekuwa hakuna mechi siku iliofuatia ili wachezaji wapate usingizi mwanana. Hata Lionel Messi anayetambulika kuwa mchezaji bora duniani hakuwachwa nje wakati wa uongozi wa Guradiola katika timu ya Barcelona. Nasri amesema kuwa hatua hiyo ilimwezesha Messi kutopata majeraha ya misuli

Andre Marriner kuchezesha mechi ya Manchester United na Arsenal

Image

Mgonjwa ashindikana kutibiwa Muhimbili kwa kuwa mrefu kuliko binadamu wa kawaida

Image
  Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida. Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya  futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake. Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao. Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya. Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili a...

Picha ya Jokate Akiwa Amekumbatiana Yazua Gumzo, Mwenyewe Adai ilikuwa Event

Image
  Watu Wabaya, Picha ya Jokate ya zamani akiwa amekumbatiana na Calisah imeubuliwa na kuzua sintofahamu huku wengine wakisema Jokate alishatoka na Mwanaume huyo ambae amekuwa gumzo kipindi hiki baada ya kutoka na Wema Sepetu na kusemekana anavujisha Picha za Faragha akiwa na Wema...

Madee ampa uhuru "DOGO JANJA" kujiunga na Weusi

Image
Ni baada ya show ya Fiesta Dar es Salaam ndipo Nikki wa Pili alisikika akimmwagia sifa kibao Abdul Kachaa almaarufu kama Dogo Janja na kudai kuwa ndiye msanii wake bora wa mwaka. Yalisikika mengi kwa upande wa Weusi pamoja na Dogo Janja ikiwemo issue ya kufanya kazi pamoja na vitu kama hivyo lakini Madee Ali ambaye ndiye mlezi wa Dogo Janja alikuwa hajasikika kokote kuhusiana na suala hilo.   imemtafuta raisi wa manzese Madee na kupiga nae story kuwa analizungumzia vipi suala hilo la Dogo Janja kufanya kazi na Weusi, na Madee alikuwa na haya ya kusema. “Hiyo ni biashara ambayo iko kwenye engo ningine kabisa, kama Dogo Janja ataamua yeye kama yeye mimi wala sitokuwa na shida kwasababu anaweza kuwa anaona kule kuna kitu ambacho atakuwa anakipata tofauti na huku ambako ameishi, me nadhani ntampa uhuru tu na kumtakia mafanikio mema. Lakini kama ni biashara nyingine ambayo hao anaotaka kufanya nao biashara watataka kufanya na Dogo Janja basi itabidi waufuate uongozi wa Tiptop Connectio...

Calisah Afunguka Baada ya Kusambaa Kwa Video yake Akimla ‘Denda’ Wema Sepetu.

Image
  eekend hii katika mitandao ya kijamii kumesambaa video inayomuonyesha malkia wa filamu nchini Wema Sepetu akiliwa denda na model Calisah. Wawili hao ambao walitumia nguvu nyingi kufanya siri mahusiano yao, wameumbuka kupitia video hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii. Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Calisah amesema hajui ni nani ambaye amesambaza video hiyo mtandaoni kwani walikuwa nayo yeye pamoja na Wema. “Nilikuwa nachati na Wema kawaida ghafla nikaona notification, kufungua ndio nikakuta hiyo video na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumuuliza Wema kwa sababu video nilikuwa nayo mimi na Wema,” alisema Calisah. Pia model huyo amedai video hiyo imemsababishia matatizo katika familia yake pamoja na kumpoteza bibi yake kwa presha.

Hizi Hapa Mbinu za Kumpata Mwanamke Yoyote Hata Awe Ngumu Vipi.

Image
  Kifupi unakuta mwanaume ana status nzuri tu lakini anakosa mwanamke anayejielewa.yaani wengine hadi wananiuliza sometimes mimi "hivi wewe unawapataje wanawake wazuri na wanaojimbua hivo". Sasa leo nimeona ni vyema nikishare na nyinyi namna ya kumnasa demu hata awe ni anajitambua vipi! 1: Unapoomba namba ya simu hakikisha huombi kwa papara, yaani usioneshe kama una shida sana na usioneshe kama unataka kumtongoza, bali onesha kama unataka tu ulafiki wa kawaida,yaani lafiki wa kuchati nae tu kawaida. 2: Akikupa namba leo kausha usimtafute leo leo, mtafute baada hata ya wiki,msalimie tu na umpigie, hapa uangalie na muda ambao unadhani mtu anakuwa free, sio kupiga simu asubuhi sana au mchana au usiku sana, piga mida ya saa mbili usiku,na usiongee nae zaidi ya dakika 5. 3: Hakikisha kila siku unamtumia msg mara 3 na kumpigia simu mara moja, yaani asbh mtakie asbh njema, mchana, jioni na usiku piga kumpa pole na heka heka za mchana, ongea nae si zaidi ya dakika 5 ili ...

Masanja Mkandamizaji Adai Anampenda Monica Mpaka Wanawake Wengine Anawaona ni Wavulana

Image
  Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji amefunguka ya moyoni kuhusu mkewe wake na kuandika yafuatayo.....

Dully Sykes adai umri na majukumu vilimfanya aipotezee bifu yake na TID

Image
Hapo zamani, Dully Sykes na TID walikuwa kama paka na panya. Na sasa Dully ameibuka na kudai umri wake na pia kuwa na majukumu mengi, vilimfanya asione umuhimu wa kuendelea na tofauti zao. Alikuwa akizungumza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Alikiba na kudai kuwa ipo siku wakikua, wataacha. “Hata mimi pia ilivyofikia kwenye age moja hivi nilikuwa na matatizo na TID, zamani. Lakini nilipoweza kukua niliacha hivyo, nilivyoanza kupata majukumu nikasahau kwamba tulikuwa na matatizo,” Dully alimweleza Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Donald Trump Kuwarejesha Wahamiaji Marekani Kwao

Image
  Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo. Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake . Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama. Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

Hii Ndio Kauli ya Basata Kuhusu Tetesi za Kuwepo Kwa Bifu Kati ya Alikiba na Diamond

Image
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ambalo ni walezi wa wasanii pamoja shughuli za sanaa nchini, limekiri kusikia tetesi ya bifu inayoendelea kati ya mastaa wawili wa muziki nchini, Ali Kiba na Diamond. Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema amesikia kuna bifu kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba lakini hawajapokea taarifa rasmi ambayo inaonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie. “Kwa upande wa serikali au BASATA tunafanya kazi kwa kuzingatia maandishi au taarifa rasmi, kwahiyo suala kuwepo kwa kutokuelewana kati ya Ali Kiba na Diamond halijatufikia rasmi,” alisema Mngereza. “Huu ni ushabiki au mashabiki ndio wanaleta haya, kwa hiyo ni ushabiki wa team hii na hii na tunaliona. Lakini kwa kuwa halijaja rasmi likija rasmi tutalishughulikia,” aliendelea kuongeza Katibu huyo. Aidha alisema, “Lakini tukikutana na wao wenyewe wapo safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata wachezaji wa Simba na Yanga w...

Vyakula 7 Hatari Vya Kuzuia Vinavyozeesha Ngozi Yako

Image
Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaainisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili na akili unajengwa na chakula tunachokula. Madhara ya chakula chetu tunachotumia yako pia katika ngozi. Kuna vyakula vinavyozeesha ngozi kwa haraka na ni budi kuvijua na kuviepuka. Vyakula hivi japo tunavipenda sana lakini vina athari mbaya kwa miili yetu na muhimu kujenga tabia ya kuviacha katika milo yetu. Kama si rahisi kuacha kabisa basi angalau kupunguza matumizi yake. Vifuatavyo ni vyakula 7 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako: 1. Nyama Nyekundu  Mojawapo ya vyakula vinavyozeesha ngozi ni nyama hasa nyama nyekundu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa nyama nyekundu inayotokana na wanyama kama ng’ombe,mbuzi,kondoo,nguruwe n.k ni mbaya kwa afya njema ya binadamu na hivyo kwa ngozi pia. Nyama nyekundu ina kemikali aina ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi. Hivyo nyama nyekundu ni mojawapo ya vyakula vibaya kwa afya ya...

Mtoto wa Mjomba Anajilegeza Kwangu Kimapenzi...Ushauri

Image
Ndugu zangu wanajamvi...kwanza naomba niulize, mtoto wa MJOMBA angu ni ndugu kivile?..Tumekuwa tukiishi na huyo mtoto wa mjomba angu kwa kipindi kirefu...mwanzoni ilikuwa kawaida tu maana alikuwa bado mdogo, ila sasahivi chuchu konzi...msambwana umenawili..kwahiyo ameanza kubadilika, muda mwingine anaweza kuwasha mziki nikipita anajisogeza tucheze huku nimbambie ila nakataa,,muda mwingine anakuja kunikaribisha chakula anaingia bila hata kupiga hodi nakuta hata nimetoka kuoga halafu dushe limeninginia yeye anaingia tu..muda mwingine anavaa kanga moko tu au akitoka kuoga anakuja chumbani kwangu hukukhanga imeloa anadai mafuta yake yameisha eti nimpe yangu ila akigeuka anatingisha...Sasa najiuliza nimle? au ntakosea?.. maana namimi ni binadamu stimu huwa zinapanda muda mwingine..Naombeni ushauri jamani..