Posts

Showing posts from January, 2017

Watu saba wahofiwa kufa maji Ziwa Tanganyika

Image
                                 Watu saba wanahofiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika baada ya boti  ya MV Ngendo Buchuma waliyokuwa wakisafiria ikiwa na tani 20 za mzigo  kutoka mjini Kigoma kwenda mji wa Kalemie Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Kongo kutoonekana kwa zaidi ya wiki moja sasa. Mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji maboti Kigoma Uwamaki Edmud Kisinja amesema boti hiyo ikiwa na wafanyakazi wanne na wamiliki watatu wa  mzigo wa vitunguu gunia 110,soda kreti 70,mafuta pipa 20 na ngano mifuko 180, waliondoka tarehe 23 mwezi wa kwanza lakini mpaka sasa hawajulikani walipo huku jitihada zikiwa zimefanywa kuwatafuta Mashariki ya DRC pamoja na upande wa Tanzania bila mafanikio hali inayoashiria huenda boti hiyo ambayo ilipaswa kutumia kati ya masaa 12 hadi 24 kufika DRC,imezama ziwani. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma kamishna Msaidizi Mwandamizi Ferdinand Mtui ame...

Mambo 6 yatakayo kufanya ukose heshima kwenye jamii yako

Image
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa. Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu. Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda. Njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa. 1. Muonekano. Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani. Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dog...

Jose Leonardo Ulloa agoma kuichezea Leicester City

Image
Mchezaji wa klabu ya Leicester City Jose Leonardo Ulloa amegoma kuendelea kubakia katika klabu hiyo baada ya kuonyesha kukasirishwa na kocha wake Claudio Ranieri kukiuka makubaliano yao na kusema hawezi kuichezea tena Leicester sababu Ranieri kamsaliti. Jose Leonardo Ulloa amesema kuwa Ranieri alisema angemruhusu kuondoka Leicester City na kwenda kujiunga na klabu nyingine endapo ingetoa ofa ya kuanzia pound milioni 4 na kuendelea, ila alishangazwa na kocha wake huyo hataki tena kuona nyota huyo akiondoka. “Kocha wiki mbili zilizopita alisema kuwa kama ofa ya kati ya pound milioni 4 hadi 5 itakuja mezani ataniruhusu kuondoka lakini ninachokifahamu nikuwa ofa zilizokuja ni za kiwango hicho na zaidi lakini anazipotezea“ Hii ni Tweet ya Jose Leonardo kwa mashabiki wa Leicester City Jose Leonardo Ulloa alijiunga na Leicester 2014, kaichezea jumla ya mechi 89 na kuifungia magoli 20. Sunderland imeonesha nia ya kumuhitaji nyota huyo na ipo tayari kutoa pound milioni 7 kwa ajili yake, Sund...

Mhubiri aliyekuwa na wake 86 afariki Nigeria

Image
Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93. Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili. Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake. Mzee mwenye watoto 70 na wajukuu 300 Tanzania Wengine wao walikuwa wajawazito. mwaka 2008 kuwa alikuwa na takriban watoto 170 lakini gazeti hilo lilisema kuwa aliwaacha watoto 203.

Wachezaji wa West Ham walimtaka Payet Kuondoka

Image
Wachezaji wa klabu ya West Ham walitaka Dimitri Payet kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuelekea Mersaille ,kulingana na mwenyekiti mwenza wa klabu hiyo David Sullivan. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 alijiunga tena na klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni milioni 25 baada ya kudaiwa kukataa kuichezea West Ham kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita. ''Kwa kweli hatukutaka aondoke lakini huwezi kwenda kinyume na umoja wa timu'' ,sullivan  Sullivan alisema kuwa Payet aliamua kutochukua mshahara wake wa Januari. ''Payet hakuzungumza na mtu kwa wiki sita.Amekataa kuzungumza na mtu yeyote katika timu'',alisema Sullivan. Payet alijiunga na West Ham mwezi Juni 2015.

Sinaga Swagga ya Young Killer ipo kwenye playlist ya Fid Q

Image
Wiki iliyopita mcee mkongwe nchini, Fid Q alizua maswali mengi baada ya kuonesha kuupa heko wimbo mpya wa Joh Makini,Waya, mkali ambaye tulikuwa tukiamini kuwa wana tofauti. Sasa mbali na ngoma hiyo ya Joh Makini,Fid Q ameitaja ngoma ya Sinaga Swagga ya Young Killer kuwa ni ngoma ambayo ameisikiliza sana pia. “Nimeiskia Sina Swagga ya Young Killer,nimeipenda, nimependa jinsi ambavyo amejaribu kuwa yeye,” Fid kwenye mahojiano nami kupiti Kings FM. Kwa muda mfupi wimbo huo wa Young Killer ulisababisha headlines kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuwachana rappers wenzake wakiwemo Joh Makini, Young Dee na Dogo Janja. By Prince Ramalove Kings Fm

Usajili wa TIN wafikia kikomo

Image
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitaongeza siku za kufanya uhakiki wa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) hapa jijini baada ya muda kumalizika leo, hivyo wote watakaokuwa hawajahakikiwa watafutiwa namba zao na watatakiwa kuomba upya. Kwa mara ya kwanza TRA imepanga kufanya uhakiki wa TIN kwa siku 60 kati ya Agosti na Oktoba lakini baada ya kujitokeza watu wengi tarehe ya mwisho iliongezwa hadi Novemba na mara ya tatu ilisogezwa hadi Januari 31. Lengo la uhakiki huo ni kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo. Kayombo alisema kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanahitaji kuhakikiwa namba, mamlaka iliamua kusogeza mbele muda wa kutoa huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya kutoa huduma ambako watumishi walifanya kazi hiyo hadi Jumamosi na Jumapili kuwapa nafasi wafanyakazi. Alisema madhara kwa watakaofutiwa TIN ni makubwa kwani wafanyabiashara na madereva wa magari leseni zao zitakuwa batili na watachukuliwa hatua kwa kosa la kufanya b...

Mvua yaezua paa za madarasa sita na choo

Image
PAA za madarasa sita ya Shule ya Sekondari Kisumwa iliyopo katika Tarafa ya Suba mkoani Mara pamoja na nyumba za walimu na choo, zimeezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo. Mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki, pia imeharibu nyumba na mazao ya wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora mkoani Mara. Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo. Chacha alisema mvua hiyo ilinyesha wilayani Rorya ikiwa ni baada ya zaidi za mwezi mzima ikikumbwa na ukame. Alisema mvua hiyo iliyokuwa imeambatana na upepo mkali, iliezua paa za madarasa sita, nyumba ya mwalimu na choo katika Shule ya Sekondari Kisumwa. Kadhalika, Chacha alisema mvua hiyo pia iliharibu mazao na baadhi ya nyumba za wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora. Alisema Kamati ya Maafa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha, itafanya tathmini ya mali iliyoharibika katika shule hiyo na kwa wakazi wa vijiji hivyo...

Mohamed Elneny nje michuano ya AFCON

Image
Kiungo wa kati wa timu ya Arsenal Mohamed Elneny anakabiliwa na jukumu la kuhakikisha ana kuwa sawa kiafya ili kushiriki katika fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu AFCON, endapo nchi ya Misri itafanikiwa kufika hatua hiyo. Elneny ni miongoni mwa wachezaji wakali wa Misri na tayari amekumbwa na tatizo la kifua wakati wa mchezo wa nusu fainali wakati timu yake ilipomenyana na Morocco. Meneja wa timu timu ya Misri Ihab Lehata amethibitisha kuwa Elneny huenda asiingie uwanjani tena katika michuano hiyo.

Waliookolewa mgodini watoka hospitali.

Image
Geita. Wachimbaji 15 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya matibabu baada ya kuokolewa katika mgodi wa RZ walikokuwa wamefunikwa na kifusi cha udongo kwa siku tano wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya zao kuwa nzuri. Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Brian Mawala amesema afya za wachimbaji hao zimeimarika na wana uwezo wa kuendelea na kazi. Baada ya kuruhusiwa leo asubuhi wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga.

Picha: Meli kubwa ya kisasa ya Azam yatia nanga Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza

Image
Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga Bandari ya Tanga leo. Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.

TFF yaguswa na Kifo cha mchezaji wa Kagera Sugar.

Image
Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF limesema kuwa limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Burhan mchezaji wa Kagera Sugar ambaye mefariki usiku wa kuamkia leo. Kupitia ukurasa wake wa twitter rais wa shirikisho ls soka Jamal Malizi aliandika haya "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar.Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani.alisema Malizi. Mapema hibvi leo taarifa za msiba wa Kipa wa Kagera Sugar, David Burhani zilianza kuvuma haswa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba amefariki dunia. David Buruhan kipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki katika Hospital ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na Malaria, Burhani aliwahi kuichezea Mbeya City na baadaye aliweza kujiunga na Majimaji ya Songea na kuitumikia msimu mmoja. aarifa zaidi endelea kufuatilia taarifa zetu.

Bastian Schweinsteiger kusalia Manchester United

Image
Bastian Schweinsteiger hataihama klabu ya Manchester United na atajumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kinachocheza ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, kwa mujibu wa meneja Jose Mourinho. Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga wakati wa ushindi wa United wa 4-0 Kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili. Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016. Schweinsteiger aliachwa nje ya kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho na akalazimishwa kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 mwanzoni mwa msimu. Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young. "Ataenda kucheza Europa League kwa sababu tumeachwa na nafasi za kujaza kutokana na kuondoka kwa [Memphis] Depay na [Morgan] Schneiderlin." Schneiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye. United watakutana na Saint-Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16 Februari, na mechi ya maru...

Magazeti ya Tanzania yameamka na hizi Leo January 30, 2017 katika Udaku, Hardnews, na Michezo.

Image
HABARINI ZA ASUBUHI..Leo ni  January  30, 2017 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania  kuanzia kwenye, Udaku, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea .. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook, twitter na instagram @boazmwakasege ili niwe nakutumia kila kinachonifikia. subscribe @YouTube Boaz  tv

Federer amshinda Nadal kwenye Australian Open.

Image
Roger Federer amepata ushinda wa 18 wa Grand Slam kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano kwa kumshinda kwa seti tano mfululizo Rafael Nadal, katika fainali ya mashindano ya Australian Open. Federer mwenye umri wa miaka 35 alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-1 3-6 6-3 na kupata ushindi wake wa tano wa Melbourne. Nadal mwenye umri wa miaka 30 yuko nafasi ya pili sawa na Pete Sampras. Ushindi mkubwa wa mwisho wa Federer ulikuwa wa Wimbledon mwaka 2012. "Nimekuwa nikija hapa kwa karibu miaka 20 sasa,"alisema. Nimekuwa nikifarahia na sasa familia yangu inafurahia pia.

Real Betis watoka sare ya 1-1 na Barcelona.

Image
Bao la Luis Suarez dakika ya mwisho liliokoa jahazi la Barcelona na kusababisha kutoka sare ya bao moja na Real Betis. Real Betis ilitawala mechi na mchango wao Dani Ceballos na Ruben Castro ukazaa matunda wakati Alex Alegria alipoutumbukiza mpira kwenye wavu. Awali bao na Barcelona lilikataliwa kutokana kutokuwepo kwa teknolojia ya kutambua bao likivuka mstari wa goli kwenye michuano ya La Liga. Hata hivyo Suarez alitumia fursa ya kipekee baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Lionel Messi dakika ya mwisho na kusawazisha . Barcelona wako pointi moja nyuma ya Real Madrid ambao wana mechi mbili za kucheza ikiwemo ya nyumbani dhidi ya Real Sociedal  siku ya Jumapili

Liverpool kumsafirisha Mane kwa ndege ya kibinafsi

Image
Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea. Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakai wa mechi za robo fainali siku ya Jumamosi. Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo. Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushirika mechi za kimataifa. Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.

Huyu Ndio Faru Fausta wa Ngorongoro, Atimiza Miaka 54, Aishi Chini ya Ulinzi wa Kijeshi Masaa 24

Image
FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54 Ndio faru mzee duniani,sasa haoni .Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54. Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo. Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba. Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua hatua juu ya Faru Fausta

EXCLUSIVE: Maalim Seif ahojiwa… kuna hii mistari yake 13 nimemnukuu.

Image
Leo January 29 2017 kupitia Funguka ya AzamTV, katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amehojiwa na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo za Profesa Lipumba, Zanzibar na maamuzi yake mengine. Kweli Lipumba alijiuzulu na alipoonyesha nia ya kujiuzulu tulimfuata kwenda kumuomba sana asiondoke hasa wakati ule tulikuwa tunakabiliwa na uchaguzi lakini akaendelea na msimamo wake, hakufukuzwa Lipumba kajiuzulu mwenyewe, amekaa baada ya miezi 10 anaandika barua kwamba anatengua jambo hili mimi sijawahi kuliona hilo Duniani Fedha za ruzuku zimekwenda kwenye akaunti ambayo bodi ya wadhamini, katibu mkuu hawaijui Ukiingia kwenye siasa lazima ukubali kutukanwa, kushambuliwa, kufungwa hata kifo, mimi yote nimeshapitia isipokuwa kifo-Maalim Seif. Jimbo la Dimani kihistoria ni la CCM na sisi tuliingia kwenye uchaguzi tukijua tuna kazi kubwa’Ulikosa? Natarajia muda mfupi ujao nitakuwa Rais wa Zanzibar’ Baada ya kuacha wadhifa safari zote za nje najilipia mwenyewe na siombi serikal...

Ni sawa rapper aliyedumu miaka 15 kushindanishwa na mwenye miaka 2 kwenye game? Haya ni maoni ya Mwana FA

Image
Mwana FA anaamini kuwa katika muziki kushindanishwa kwa wasanii ni kitu ambacho hakiwezi kuepukika. Na katika miaka ya hivi karibuni ambapo shabiki ana access ya kukosoa, kusifia au kushindanisha, ndio imekuwa balaa kabisa, lakini hakukwepeki. “Leo Mwana FA akitoa wimbo mzuri, watakuambia Mwana FA mkali kuliko fulani na fulani, kuna watu watakuambia MC fulani sababu ametoa wimbo sasa hivi, wimbo wake mkali basi MC fulani ndio mkubwa kuliko mamcee wote waliowahi kutokea nchi hii. Kama wanavyosema, opinion sio kitu ambacho mtu anaweza kushtakiwa kwa kuwa nacho, unless ni za kisiasa ama zina matatizo kwenye usalama wa taifa na vitu kama hivyo, lakini kila mtu anaruhusiwa kuwa na zake na hatuwezi kukulazimisha ubadilishe opinion zako,” FA amesema tatizo pekee katika uhuru huo wa kujieleza na kuwa na majukwaa mengi ya kutoa maoni, watu ambao hawana uelewa wa kutosha katika kile wanachokielezea, hupotosha ukweli. “Mfano halisi ni hili tunalolizungumzia, kuna watu hawajui muziki, wengine wame...

Waliotafuna zaidi ya shilingi bilioni 1 za ushirika washughulikiwe -Majaliwa

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na upotevu zaidi ya shilingi bilioni moja za vyama vya ushirika. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Januari 27, 2017) alipozungumza na watumishi wa Mkoa wa Njombe wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani hapa. Alisema kati ya fedha hizo sh. milioni 532.736 zilipotea katika SACCOS ya Kurugenzi Njombe pamoja na sh. milioni 900 zilizopotea katika Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kiitwacho Wafanyabiashara Njombe SACCOS. “Maofisa Ushirika nchini mmeendelea kudhoofisha jitihada za Serikali katika kuimarisha ushirika. Katika eneo hili ninahitaji Mkuu wa Mkoa ufuatilie suala hili na kuwachukulia hatua wahusiuka wote,” alisema. Waziri Mkuu aliwaagiza Wakuu wote wa Wilaya kuwatumia warajisi wa ushirika kuimarisha ushirika Mkoani Njombe.”Tunataka ushirika ulete tija kwa wananchi na hatutaki ushirika ulioambatana na harakati za...

Alikiba, yazingatie malalamiko ya mashabiki wako.

Image
Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act. Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda. Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria. Ushindi wa MTV EMA pia ambao awal...

Picha: Dunia yampinga Trump baada ya kupiga marufuku kwa Waislamu kuingia Marekani

Image
Uamuzi wa Donald Trump kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo, umesababisha hasira kuu duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani. Raia waliokuwa na hati za kusafiria kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege, wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege walishikiliwa baada ya kutua Marekani. Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni, waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi kwenye nchi zao. Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka 2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. Rais Trump amepiga marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi wa kiislamu wasiingie nchini humo. Wakimbizi kutoka Syr...