MAKUBWA Yafichuka Faru John

Maofi sa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maofi sa Taasisi ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wakiwamo madaktari, wakifanya uchunguzi wa Faru John baada ya kufa katika eneo la Sasakwa Grumeti. SAKATA la kutoweka kwa faru John lililoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mikoa ya Arusha na Manyara linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha. Taarifa zilizolifikia MTANZANIA baada ya kufanya uchunguzi wa sakata hilo kwa wiki kadhaa sasa, zinaonyesha kwamba uamuzi wa kumhamisha faru huyo kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ulihusisha mamlaka za kitaifa za Serikali. Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba mchakato wa kuhamishwa kwa faru John kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kwenda Grumeti, ulianza katika eneo la Nyasirori ndani ya Hifadhi ya Serengeti Aprili 17, 2015. Uamuzi huo kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika serikalini, ulianza siku hiyo...