Posts

Showing posts from August, 2016

(VIDEO+PICHA) Ajali ya basi kampuni ya SATCO na PRADO, zagongana Mkoani singida.

Image
Asubuhi ya August 29 maeneo ya kona ya stendi mpya iliyopo Singida mjini imetokea ajali ya basi kampuni ya SATCO na gari ndogo aina ya PRADO … Gari ndogo hiyo imegongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Dodoma. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo gari ndogo ilikuwa  ikiendeshwa na mwanaume ambaye hakuweza kuzurika na MWAKASEGE BLOG  bado inafuatilia kwa kina taarifa kutoka jeshi la polisi.       

Mwimbaji Ruby Akimbilia EFM Radio Baada ya Ugomvi wa Maslahi Kati ya Mwimbaji Huyo na Clouds FM

Image
Mwimbaji Ruby ambae alikuzwa na kulelewa na Clouds FM Baada ya Kufanya vizuri katika mashindano ya Fiesta Diva Nyota miaka kadhaa iliyopita amejikuta katika ugomvi wa kimaslahi na walezi wake Clouds FM baada ya kushindwana malipo katika Matamsha ya Fiesta yanayoendelea hivi sasa.. Ruby kwa sasa inaonekana amekimbili kwa washindani wa Clouds FM ambani ni EFM Radio, Radio hiyo mpya ambayo ni washindani wa Clouds FM kwa jijini Dar es Salaam wamechukua fursa hiyo na sasa wanamtumia katika matamasha yao ya Mziki Mnene Sehemu mbali mbali... Je unaona ni sahihi Ruby Kufanya hivyo?

DK TULIA- HAKUNA ANAYEPENDELEWA BUNGENI,WABUNGE WOTE NI SAWA

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema hakuna Mbunge ambaye ana hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge, bali katiba inawatambua wabunge wote wapo sawa. “Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa” Amesema Dkt. Tulia Aidha Naibu Spika ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa. “Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii” Amesema Naibu Spika Dkt. Tulia. Kwa upande mwingine Naibu Spik...

PESA ZA ELIMU BURE ZAANZA KUTAFUNWA

Image
FEDHA zilizotengwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kugharimia elimu ya bure nchini, zimeanza kutafunwa baada ya kubaini kuwapo kwa udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu kwa kuongeza idadi ya wanafunzi hewa ili kupata fedha zaidi. Kutokana na hali hiyo, wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Manispaa ya Arusha, zimebaini udanganyifu huo na kuchukua hatua za awali kwa kusimamisha walimu wakuu wa shule husika na pia kuziagiza mamlaka husika kuwavua uongozi walimu hao. Hivi karibuni, Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa wilaya zote, kushughulikia udanganyifu unaofanywa na walimu wakuu wanaotafuna fedha kwa kuweka wanafunzi hewa katika suala la elimu bure baada ya serikali kuanza kutoa elimu bure Januari mwaka huu, ikitenga Sh bilioni 18.7 kila mwezi. Wanafunzi hewa Kinondoni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa kubainika kwa wanafunzi hao kumekuja baada ya kuagiza mkurugenzi na watendaji kufanya uhakiki shule kwa shule ili kuba...

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wenzake 8 Wafikishwa Mahakamani

Image
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine  nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea. Mnamo mwezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo. .

Taarifa za awali za Polisi Dar baada ya kuwakamata Original Komedi

Image
August 17 2016 Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imewahoji wasanii wanne wa kundi la sanaa ya uigizaji Orijino komedi akiwemo kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.  Kaimu kamishna wa jeshi la polisi Dar es salaam Hezron Gyimbi ambaye ametusogezea taarifa za awali kwa kusema…>>> ’Wamekamatwa jana saa 10 jioni ambapo wamehojiwa na wamekaguliwa sehemu wanazokaa kuona kama wana vitu zaidi ya uniform‘ ‘Tunakamilisha hatua za kiupelelezi, makosa yanadhaminika wakipata watu wanaweza wakawadhamini sababu dhamana ni haki ya mtu‘-Hezron Gyimbi

SUPER STAR JACKLINE WOLPER NA HARMONIZE WATIKISA KWENYE BIRTHDAY YA DJ WA DIAMOND PLATINUMS

Image
kuona utamu wote   ==> BONYEZA HAPA

Zifahamu Sababu za Justine Bieber Kufuta Account yake ya Instagram

Image
Moja kati ya mastaa wanaongoza kuwa na Followers wengi katika mitandao ya kijamii huwezi kuaacha kumtaja Justine Bieber ambaye account yake ya Instagram ina jumla ya wafuasi milion 77.8 , Mtu wangu headlines zimechukuliwa leo na Staa huyo anayemiliki hitsong ya ‘Sorry‘ kuamua kuifuta account yake ya instagram Kisa kimeanzia pale Justin Bieber alipokuwa anapost picha na msichana ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Lione Richie mwanamitindo Sofia Richie mwenye umri wa miaka 17 ambapo ameonekana akiwa na Justin Bieber kwenye mitoko mingi hivi karibuni. Baada ya Justin Bieber kupost picha akiwa na msichana huyo mashabiki wake wamekuwa wakicomment maneno yalioonesha kuwa ya chuki na kutopendezwa kwa Justin kuwa karibu na msichana huyo, maneno yalivyozidi Justin akaamua kupost picha na kuandika maneno haya … ’Nitaifanya account yangu iwe private kama hamtaacha chuki, kama nyie kweli ni mashabiki zangu hamuwezi kuchukia watu ninaowapenda mimi‘ Mkasa ukazidi pale mwanamuziki Selena Gomez ambae ni E...

Peter Msechu Aingia 18 za AT, Achambwa Mpaka Huruma...

Image
Mwimbaji AT kutoka Zanzibar amemtupia Mwimbaji Peter Msechu Maneno ya Shombo ambayo yamemwacha kila mtu mdomo wazi: “Mvuto Sifuri Bikaka @peter_msechu Nene km Lori Hivi kuongelea wembamba wangu unalipwa sitaki shobo km lakufanya huna jikate minyama yako ujichome mishkaki usi nitekenye mdomo ukataka niongee,” ameandika AT kwenye Instagram. “Tumbo Tumbo km Umeficha Kobe wewe nipotezee usilazimishe mimi niwe karibu na wewe sina shida ya kukuazima tumbo nende nalo harusini Mifulana km Turubali za Msimbani Babu kaa mbali na mimi kwani hivi na wewe ni msanii wanchi hii au Muuza kufia za Oliva Mtukuzi?” “Pyuuuuuuuuuuuuu ukiona nipo kimya ujue sihitaji varangati na mtu kiki zime adimika huna utakapopatia usinione Mwembamba ingia 18 uhadithie wenzio Mr Machupi ya kushonesha.” JE ULIPITWA NATUKIO ZIMA LA HARUSI YA MASANHA MKANDAMIZAJI??? HII HAPA MTU WANGU NIMEKUSOGEZEA. 

Walichokusudia Kufanya Wanachama wa Yanga Leo Kuhusu Yusuph Manji Kuibwaga Yanga

Image
Baada  ya taarifa za mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuripotiwa kukusudia kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya klabu ya Yanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuandamwa na maneno na baadhi ya watu huku wana Yanga wengine wakiwa kimya. Taarifa za Manji kujitoa zinakuja kwa sababu ya kudaiwa kujihisi mpweke kwani licha ya kushambuliwa kwa maneno na baadhi ya ya watu ikiwemo wanasiasa, hakuna mwanayanga aliyekuwa pamoja nae hivyo anajihisi mpweke na ana kusudia kujiweka pembeni. Kufuatia taarifa za Manji kukusudia kujitoa viongozi wa Yanga wa kanda zote wamekusudia kufanya kikao leo saa 4 asubuhi makao makuu ya klabu hiyo kutoa tamko la pamoja kuhusiana maamuzi ya Manji, kujitoa kwa kuona anatengwa na wanachama.

(PICHA) MREMBO ALIYEHIT HUKOO INSTAGRAM.....

Image
👏 beautifull babies ..📷📷 Follow 👉 @boazmwakasege8 A photo posted by Boaz Mwakasege (@boazmwakasege8) on Jul 26, 2016 at 5:40am PDT

HATIMAYE Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji Afunga Ndoa(PICHA)

Image
MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ , Jana ameuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu aitwaye Monica. Ndoa hiyo imefungwa katika Kanisa la Mito ya Baraka lililopo Jangwani jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi huyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Tulia Ackson.

Watu 30 Wauawa Kinyama Mashariki mwa Congo DRC

Image
Ripoti kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zinasema kuwa wanajeshi wamepata miili ya takriban raia 30 waliouawa katika shambulizi mashariki mwa taifa hilo. Msemaji wa jeshi Mark Azuray ameambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo yalitokea katika mji wa Beni nyakati za usiku. Wanajeshi wanashuku kuwa kundi la wanamgambo la ADF lilitekeleza mauaji hayo. ADF ni kundi la kujihami lililo na asili yake nchini Uganda, na linaendeleza shughuli zake karibu na mpaka. SOMA CHANZO CHA BIFU LA VERA NA HUDDAR, BONYEZA HAPA CHINI.

Hiki Ndicho Chanzo Cha Bifu la Vera na Huddah

Image
Mrembo kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu ya kuwa na bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe, bifu ambalo limeteka vyombo vya habari kwa muda mrefu Akifunguka kwenye FNL ya East Africa Tv na Radio , Vera Sidika amesema wakati yeye akiwa Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu jijini Nairobi, lakini alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki, lakini baadaye Huddah alionyesha kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi, kwani alihisi anamchukulia nafasi yake kwenye kazi. "Bifu ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari alishakuwa star, na mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama nimeingilia career yake, ikawa anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo sitaki lakini anayaleta tu", alisema Vera Sidika. Vera aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale inapofikia hatua ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za uongo, akitolea mfano wa hivi ...

Mzee Yusuf Afanya Maamuzi Magumu

Image
Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuf amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita. Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa mwanamziki huyo ameachana na mziki na kuamua kumrudia Mungu. Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu usiku huu, mmiliki huyo wa bendi ya Jahazi Modern Taarab amethibitisha kuwa taarifa hizo ni kweli na kuongeza: “Nashangaa taarifa hizi zinasemwa leo. Ni suala la muda mrefu….takribani miezi miwili iliyopita na sababu ni kuwa nimeamua kumrudia Allah,” Mwanamziki huyo mzaliwa wa Zanzibar alipoulizwa kuwa ni suala gani lililomsukuma hata achukue maamuzi hayo magumu, alijibu kwa kifupi, “ndivyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini.” Yusuph aliyetamba na vibwagizo kama “Nichumu, nikisi….mwaaaa,” katika baadhi ya nyimbo zake, amesema familia yake imeupokea uamuzi wake kwa mtazamo chanya na kwamba inamuunga mkono. “Kwa sasa nitaimba kaswida zenye mafundisho ya dini,” amesema nyota huo huku akiahidi kufanya...

Ridhiwani Kikwete Awapongeza AliKiba na Diamond ‘Mmeonyesha Umuhimu wa Kuwa Mastaa’

Image
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa muziki, Diamond Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni kwa ‘GSM Foundation’ ili kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi. Diamond na Ali Kiba Mtoto huyo wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia matatizo ambayo yanatokea katika jamii. “Katika vitu vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni hili mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa kwa kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani aliandika katika instagram yake. Aliongeza, “Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii yetu yenye mahitaji. Peace to you,” Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi hiyo wa tsh 20 Milioni na baadae AliKiba na yeye aliamua kuto...

HUYU NDIYE MPENZI WA JASON DERULO ALIYE ACHIA PICHA ZA NUSU UTUPU MTANDAONI

Image

MREMBO VICTORIA KIMANI AACHIA PICHA ZA NUSU UTUPU(+PICHAZ)

Image

STAA ALIKIBA ASHINDA TUZO MBILI HUKO USA

Image
staa Alikiba ambaye kwa sasa yupo chini ya Sonny Music ameshinda tuzo mbili katika tuzo za Holly Wood $ African People's Choice zinazofahamika kama THE NAFCA zilizofanyika Califonia USA, Alikiba alikuwa akiwania tuzo hizo katika vipengele viwili 'Favorite Artist of the year'na Favorite song of the year.

MAHUSIANO NA NDOA- NIPO KWENYE NDOA MWAKA SASA ILA MICHEPUKO INANISUMBUA NAOMBENI USHAURI!

Image
Mimi ni mwanamke niliye kwenye ndoa ya mwaka mmoja na miezi7, kabla ya kuolewa na huyu mume wangu nilikuwa na mahusiano na kijana mmoja ambae tulipendana na kushibana sana ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu hatukuweza kuoana. Baada ya kuachana(kwa amani kabisa) ndipo nikampata huyu ambae ni mume wangu sasa, nae(ex) alipata mwanamke akaoa. Baada ya muda wa miezi 7 ya ndoa yangu na ya ex ikiwa na miezi mitatu tulianza tena mawasiliano maana hakuna aliyeweza kumsahau mwenzake, na sio siri sijawahi penda mwanaume kama nilivyompenda ex (i have even his pic in my wallet nikimmiss naicheki najikuta tu naloa) Kwahiyo tukawa tunakumbushiana ila baadae tukanogewa ikawa kwa wiki lazima tuonane hata mara tatu, and to be honest he is good on bed than my husband, yaani anajua kunikuna haswaaa. Sasa nina ujauzito wa miezi mitatu na ktk kupiga mahesabu nikagundua ni ya ex, hivyo nikaamua kukata mawasiliano nae kabisa, mume wangu alipogundua am pregnant alifurahi kupita maelezo maana awali...

SAMIA- OLE WENU MAFISADI WA FEDHA ZA MIRADI

Image
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano, itapambana kwa nguvu zote na vitendo vya ufisadi kwenye fedha, zinazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Amesema serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kudhibiti matumizi yasiyo lazima na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa, zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi. Alisema hayo jana wakati akifunga maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane kitaifa katika Uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa niaba ya Rais John Magufuli. Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Makamu wa Rais alisema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia, iwapo tu vitendo vya ufisadi katika fedha zinazoelekezwa kwenye maendeleo utakoma. Alisema pia hayo yatawezekana endapo wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati...

JPM- WATANZANIA OMBEENI AMANI

Image
Rais Magufuli alisema pamoja na Watanzania wote kuungana kuombea amani na utulivu, pia hawana budi kutekeleza kwa vitendo maandiko matakatifu ya Biblia yasemayo “Asiyefanya kazi na asile” kwa kuhakikisha kila mmoja anachapa kazi kwa juhudi na maarifa ili kuharakisha maendeleo ya Taifa. “Ndugu zangu nawashukuru sana, muendelee kuliombea taifa hili, taifa letu ni la umoja, sisi wote ni Watanzania, tuendelee kumuomba Mola wetu, kudumisha amani yetu, kujenga umoja wetu kwa dini zote, makabila yote na vyama vyote, kwa sababu Mola wetu anatupenda sisi sote,” alisema Rais Magufuli. Aidha, baada ya kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Rais Magufuli aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la kanisa hilo, ambapo Sh milioni moja zilikusanywa papo kwa hapo. RAIS John Magufuli ametembelea msikiti na makanisa yaliyopo Chato mjini mkoani Geita na kuendelea kuwasihi Watanzania kuombea amani na utulivu katika nchi, bila kujali tofauti za dini, makabila ...

GALLERY: UNITED'S 20 COMMUNITY SHIELD WINS

Image
Manchester United will play in a record 30th Community Shield match this weekend, having played in the very first fixture of its kind back in 1908. The Reds won that one and have 20 successes in total on the honours board - 16 outright triumphs and four shared after a draw. Introduced as the FA Charity Shield in 1908, it had evolved from the Sheriff of London Shield match, which was played between a top professional side and a leading amateur team. This format was maintained when United, the reigning Football League champions, beat Queens Park Rangers, the then-Southern League champions, 4-0 in a replay after the first match had ended 1-1. Both games were at Stamford Bridge. This format, with the occasional representative side taking part, was to form the basis of the competition for many years. It wasn't until 1974 that the fixture was established as we know it today - a contest between the league champions and the FA Cup winners, played at Wembley as proposed by the then-FA secre...

CHANZO CHA USALITI KWA MWANAMKE

Image
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe. Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla. Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa UKOSEFU WA MAHABA Kwa asili mwanamke anasilika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.. Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji ...

birthday ya mtoto wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu kamuandikia ujumbe huu.

Image
Leo August 6, 2016 ni siku aliyozaliwa mtoto wa staa wa bongo fleva Diamond Platnumz ambapo watu wengi wamemtakiwa mtoto huyu kila la kheri kwenye Birthday yake, bongo movie staa aliyewahi kuwa na mahusiano na Diamond ‘Wema Sepetu‘ hakuwa nyuma kwenye salamu za heri ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto huyu, Wema Sepetu aliandika hivi instagram>>>“ Happy Birthday Princess Tee…???????????????????????? May Allah bless your precious lil self… You will definitely turn out to be a phenomenal young woman “

UEFA: IMETANGAZA TOP 3 YA WACHEZAJI WATAKAO WANIA TUZO YA UCHEZAJI BORA BARANI ULAYA.. MESSI NJE.

Image
Shirikisho la soka barani Ulaya licha ya kuchezesha droo ya mechi za play offs za Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitangaza majina matatu ya wachezaji wa waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya 2015/2016. UEFA wamewatangaza wachezaji watatu ndio wamefanikiwa kuingia katika TOP 3 ya mwisho kati ya wachezaji 10 waliokuwa wamechaguliwa mwanzoni, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale wa Real Madrid na Antoinne Griezman wa Atletico Madrid ndio wamefanikiwa kuingia TOP 3. Washiriki wengine 7 na point zao walioshindwa kuingia TOP 3 Waandishi wa habari kutoka nchi 55 wanachama wa UEFA wanatarajiwa kupiga kura August 25 2016 kumchagua mchezaji bora wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016.

PREZZO AFUNGUKA JINSI UHUSIANO WAKE NA DIVA ULIVYOKUWA

Image
Kumewahi kuwa na tetesi miaka ya nyuma kuwa msanii wa rap toka Kenya, Prezzo alikuwa anatoka kimapenzi na mtangazaji maarufu wa clouds FM,Diva kutokana na ukaribu waliokuwa nao mpaka kufikia hatua ya mtangazaji huyo kujichora tattoo ya Prezzo. Alipoulizwa kuhusiana na tetesi hizo kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Prezzo alidai kuwa yeye na Diva zaidi ya kuwa washikaji hawajawai kujihusisha kwenye mambo ya mapenzi kama watu wengi wanavyodai. “Mimi na Diva hatukuwahi ku date,tulikuwa washikaji.Sema bloggers wanaongeza chumvi kwa sababu tulikuwa close friends ila hatujawai ku date hata denda sijawahi kula bado” alifunguka Prezzo. Alipoulizwa suala la mtangazaji huyo kujichora tattoo yake Prezzo alisema,”Alijichora tattoo si kwa vile mimi ni mshkaji wake,haimaanishi kulikuwa na kitu zaidi ya urafiki,kama ningekula vitu ningekula vitu ningesema tu sasa hivi“. Moja ya picha iliyowahi kusambaa na kuchochea tetesi za wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi

GUARDIOLA: NAISUBIRI KWA HAMU MECHI YA KLABU BINGWA.

Image
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mechi ya timu hiyo ya kufuzu kwa kombe la klabu bingwa Ulaya ni mechi muhimu zaidi msimu huu. Itakuwa aibu kubwa kwa klabu hiyo na meneja wake mpya iwapo itashindwa kufuzu. Kati ya klabu tano ambazo City huenda wakakutana nazo ni klabu ya AS Roma pekee ambayo ilikutana nayo katika mechi za makundi mwaka 2014-15 ikipata sare katika uwanja wa Etihad na baadaye kupata ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Stadio Olimpiko kufuatia mabao ya Samir Nasri na Pablo Zabaleta na hivyobasi kufuzu katika robo fainali ya michuano hiyo. City haijawahi kucheza dhidi ya Steaua Bucharest,Monaco ama Rostov ,lakini imecheza na timu kutoka Romania,Ufaransa,Urusi katika historia yao ya Ulaya. AJIBU AWEKA REKODI MPYA SIMBA, SOMA HAPA CHINI.

WAKAMATWA WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA

Image
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limekamata silaha moja ya kivita na risasi 122 zilizokutwa na watuhumiwa nane wakiwa na silaha nyingine za jadi walizo tumia kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Njombe na Iringa. Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protas akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa watuhumia hao walikutwa na silaha ya kivita yenye darubini aina ya long riffle, huku akizitaja silaha za jadi kuwa ni pamoja na shoka na nondo zinazodaiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya wizi. Silaha ya aina hiyo inakamatwa ikiwa ni mara ya pili tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo silaha zote zimekamatwa wilaya ya kipolisi Makambako na watuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi wa jeshi hilo utakapo kamilika. Aidha inadaiwa watuhumiwa hao walikutwa na dawa ya meno pamoja na mafuta ya kupaka. CHANZO: MTEMBEZI.COM