Posts

Showing posts from June, 2017

Hii video mpya ya Kendrick Lamar ‘Element’ itazame hapa

Image
Baada ya kupiga show kwenye tuzo za BET na rapa Future, Kendrick Lama r ametoa video yake mpya ‘Element’ kutoka kwenye album ya DAMN.

Michelle Rodriguez atishia kuaga filamu za Fast & Furious

Image
Mwigizaji maarufu HollyWood Michelle Rodriguez ametishia kuaga filamu za Fast & Furious kupitia IG yake huku mashabiki wakimwaga comment za kumuomba asiondoke. Michelle Rodriguez amekuwa na filamu hizi toka mwazo wa The Fast & the Furious , ila kuna tetesi kuwa anaweza asirudi tena kwenye toleo la 9 na 10. Michelle Rodriguez   aliandika hivi kwenye IG yake “F8 is out digitally today, I hope they decide to show some love to the women of the franchise on the next one. Or I just might have to say goodbye to a loved franchise,It’s been a good ride & Im grateful for the opportunity the fans & studio have provided over the years… One Love.” Akimaanisha >> F8 imetoka digitally leo, nategemea watatuonyesha mapenzi zaidi waigizaji wa kike kwenye toleo lijalo lasivyo nitabidi niache filamu inayopendwa zaidi, nashukuru kwa nafasi niliyopewa na studio hii, mashabiki, One Love“ Fast & the Furious 9 na 10 zimesha dhibitishwa kutolewa April 19, 2019, ...

Hii video mpya ya rnb staa Tamar Braxton ‘My Man’ itazame hapa

Image
Baada ya kufanya show kwenye tuzo za BET , Tamar Braxton ametoa video ya wimbo wake mpya ‘ My Man’ itazame hapa…

Ujumbe wa Vanessa Mdee kwa Jux, Atupa Dongo Gizani

Image
            Ni jambo zuri ukiona mtu wako wa karibu amefanikisha moja ya ndoto zake katika maisha yake. Ni muhimu kumpatia ujumbe ambao utakaomtia moyo katika kufanikisha mambo yake mengine aliyoyapangilia. Vanessa Mdee ameamua kutumia vizuri fursa hiyo katika kumpongeza mpenzi wake Jux ambaye amehitimu masomo yake huko nchini China. Lakini katika ujumbe huo pia Vee amewapiga dongo watu waliokuwa wakimkejeli mwenza wake huyo kutokana na muimbaji huyo kutoonyesha picha yoyote akiwa na wanafunzi wenzake. Kupitia mtandao wa Instagram, Vanessa ameandika: Congratulations @juma_jux U finally done ✅ and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE 🙌🏾👌🏾🎊

Mganga Aua, Aondoka na Kiganja Cha Mkononi

Image
WATU watatu wamefikishwa mahakamani akiwemo mganga wa kienyeji kwa tuhuma za mauaji ya Elizabeth Charles (45), mkazi wa kijiji cha Tambalale kata ya Nsimbo wilayani hapa. Waliofikishwa mahakamani hapo ni Juma Idd(25), Tatu Juma (20) wote wakazi wa kijiji cha Tambalale pamoja na mganga wa kienyeji, Shida Mwanansimbila (54) mkazi wa kijiji cha Kipungulu kata ya puge wilayani Nzega. Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya, Mengo Kamangala alidai mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Ajali Milanzi kuwa Mei 25 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku katika kijiji cha Tambalale Tarafa ya Nsimbo wilaya hapa, washitakiwa wote kwa pamoja walimpiga kisha kumuua na kuondoka na kiganja chake cha mkono wa kulia. Alisema washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo. Hata hivyo, washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo ambapo kesi hiyo ime...

Part 2, Exclusive, Jacqueline Wolper; sijatembea na Mh Makonda, mke wake ni mshauri wangu mkubwa na

Image
Muendelezo wa mahojiano ya Jacqueline Wolper kuhusu kutembea na Mh Paul Makonda , Wolper anasema Mke wa Mh ni rafiki na mshauri wake, yeye sio mwizi….

Jarida la PEOPLE na TMZ wameripoti kuwa Beyonce na Jay Z wamepata watoto mapacha.

Image
Tovuti ya TMZ imeripoti mapema leo kuwa Beyonce na Jay Z wamepata watoto mapacha. Hii imekuwa stori kubwa wiki nzima huku mashabiki wakisubiri lini Beyonce atajifungua. Watoto hao wawili wa The Carters wamezaliwa kwenye hospitali mjini Los Angeles. Mpaka sasa haijulikani jinsia za watoto hao, palikuwa na tetesi ni mvulana na msichana, ila hakuna ushahidi tosha wa kupitisha hilo… Jay Z na Beyonce tayari wana mtoto wa miaka mitano, Blue Ivy  

Jaden Smith ajigeuza Bruce Wayne kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Batman’ itazame hapa…

Image
                                        Mtoto wa Will Smith, Jaden Smith ajigeuza Bruce Wayne kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Batman‘, kwenye video hii Jaden kava suti nyeupe badala ya nyeusi kama anayovaa BatMan. Video imefanyika kwenye eneo maarufu duniani la Hollywood Walk of Fame.

Picha ya Utupu ya Amber Rose Yafutwa..!!!

Image
                                           Mtandao wa kijamii wa Instagram wenye watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani umefuta picha ya utupu ya mwanamitindo Amber Rose. Picha hiyo ambayo Amber aliiweka kwenye mtandao huo, ilifutwa kutokana na kukosa maadili. Mara nyingi mtandao huo huziondoa picha ambazo zinaripotiwa kutokuwa na maadili. Baada ya kufutwa picha hiyo ya utupu ambayo imewatoa udenda vidume wengi mitandaoni, Amber ameandika ujumbe mwingine kwenye mtandao huo unaoonyesha masikitiko yake baada ya kufutiwa picha hiyo huku mashabiki wakimuunga mkono kwa kitendo hicho.

Mara moja tu Kanye West alikubali amekalishwa kwenye wimbo ilikuwa

Image
Rapa Kanye West ni miongoni mwa wasanii watukutu sana kwenye swala la kukubali kushindwa kwenye jambo lolote, kila kitu kwake ni mashindano…. Kwenye interview kuhusu album yake ‘My Beautiful Dark Twisted Fantasy‘ Kanye West aliweka wazi kuwa vesi ya #NickiMinaj kwenye wimbo wa #Monster ilikuwa bora kuliko yake nakusema “She kicked my ass, on my own song, on the best album of the last 25 years. ” >>Kanifunika kwenye wimbo wangu mwenyewe, katika album bora ndani ya miaka 25. Moster ilikuwa na vichwa kama Kanye West,Nicki Minaj, Jay Z, Rick Ross na Bon Iver kwenye album ya My Beautiful Dark Twisted Fantasy iliyotoka mwaka 2010

Kutoka IG ya WCB Star Harmonize, ni taarifa kuwa anategemea kupata mtoto wake wa kwanza….#Hongera

Image
Kutoka IG ya bongo fleva Super staa Harmonize, ni taarifa kuwa anategemea kupata mtoto wake wa kwanza. Post yake Instagram leo June 4 2017  Inasema ” Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua😁…Chonde mtoto chukua vyote kwangu ila kwenye rangi jitahidi uibe ya mama yako…..!!! nikavimbe Mtwara 😊”

Msanii wa Wcb Harmonize aachia Picha ya Mpenzi wake Mpya.

Image
Baada ya Kuachana na mrembo wa filamu Tanzania Jacqueline Wolper, ilisemekana kuwa WCB super staa Harmonize anampenzi mpya, mzungu , ana pesa, kamnunulia gari Harmonize na anamjengea jumba kubwa huko Madale

DJ Khaled ametangaza ujio wa colabo yake na Drake

Image
      DJ Khaled ametangaza ujio wa colabo yake na Drake , wimbo huu umeitwa “To the Max.” na kava la wimbo ni picha ya mtoto wa kiume wa Dj Khaled ‘Asahd’. Wimbo huu upo kwenye album ya Dj Khaled Grateful ,humo watasikika wasanii kama from Beyoncé, Jay Z, Drake, Justin Bieber, Chance the Rapper, Lil Wayne, Quavo, na ,Rihanna.

Mimi Mars Amkana Dada Ake Vanessa Mdee

Image
Msanii anayechipukia kutoka 'Mdee Music' Mimi mars amefunguka na kuweka wazi kwamba hataweza kushirikiana na dada yake Vanessa Mdee katika kuandaa kazi ya pamoja kwa kipindi hiki kwa sababu ya mashabiki zake bado wanashindwa kutofautisha sauti zao Mars ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la 'Dedee' amesema kwa sasa yupo kwe wakati mgumu wa kujitofautisha na dada yake huyo kwai sauti zao zimekuwa zikiwachanganya mashabiki zao kiasi cha kuonekana kama Vanessa. Akizungumza na eNewz ya EATV Mars amesema kwamba "Mission yangu ni kujitahidi kubadilisha suala la kufanana na Vanessa, kwani mashabiki na watu wengine wamekuwa wakisema tunafanana uimbaji . Nadhani kwa sababu bado ni mapema hawajazoea kwani mimi ni mgeni lakini niyahakikisha nakuwa tofauti ila ikishindikana kubadilika, nadhani watakuwa wameshazoea na hata kututofautisha wao wenyewe. Lakini niwe mkweli Vanessa siwezi kufanya naye kazi sahivi mpaka watu waweze kututofautisha ...

Picha za Beckham Akiwa Mbugani Zawatoa Mapovu Wasanii wa Bongo..Lulu Amvaa Kichwakichwa Bila Kujielewa..!!

Image
  David Beckham anaonekana kuwachanganya baadhi ya watu kwa kitendo chake cha kupost picha mitandaoni bila kutaja kama yupo katika moja ya mbuga hapa nchini Tanzania. Beckham alitua nchini kimya kimya wikiendi iliyopita majira ya usiku akiwa ameongozana na familia yake na kuelekea mahali pasipo julikana huku baadhi ya wadau wakidai alikuwa ameelekea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro. Kitendo hiko kimewafanya watu kumshambulia kwenye kila picha aliyopost mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza. Hata baadhi ya mastaa wa Bongo wameonekana kushangazwa na kitendo hicho huku wengine wakitoa yao ya moyoni kupitia mtandao wa Twitter, kati yao ni Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Mwasiti. “Mbona hatoi Taarifa kwa wenye nchi Yetu🤣🤣🤣🤣atajuta nipe username yake kwanza 🤣🤣🤣🤣hata simfologi,” ameandika Lulu. Naye Mwasiti ameandika, “😂😂 huyu beckham huyu..sasa sisi ni mwendo wa kuweka bendera yetu 🇹🇿🇹🇿 tu kwenye kila picha yake mbugani kagoma kusema alipo 😂😂@OfficialLizyM.” ...

Makontena Mawili Yakamatwa Bandari Kavu AMI Dar na Madawa ya Kulevya..!!!

Image
bbbbbbbbbbbbbbb  Katika hali ya kushangaza makontena mawili yamekamatwa bandari kavu AMI Dsm yakiwa na material zakutengenezea madawa ya kulevya yaliyoagizwa na kupakiwa toka india kwa meli za CMA. Maajabu ni kwamba makontena hayo yamepitaje bandari zote mbili, India na Dsm bila kuonekana kwenye vifaa vya kitaalam bandarini humo?